Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICK

WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICK

Dodoma Investiment

Dodoma, Juni 15, 2026

Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wamepongeza uwekezaji uliofanywa na Serikali kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) katika Kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro (KLICL).

Pongezi hizo zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge mbalimbali wakati wa semina iliyoandaliwa na Wizara ya Kazi, Ajira na Mahusiano mahususi kwa PSSSF na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika maeneo ya uwekezaji na huduma, semina hiyo ilifunguliwa na Naibu Spika wa Bunge,Mhe. Daniel Sillo.

Naibu Spika wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Daniel Baran Sillo (katikati) akiendesha semina (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Bi. Zuhura Yunus na (kulia) Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Bi. Hawa Mchafu

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akifuatilia mada wakati wa semina

“Uwekezaji huu katika KLICL ni bora na kiwanda hiki ni kikubwa kuliko chochote katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, tuhakikishe tunakuwa na bidhaa bora sokoni na kiwanda kiendeshwe kibiashara” alishauri Mhe. Mabula Mgangila, Mbunge wa Msalala.


Kiwanda cha KLICL kipo mjini Moshi na kinamilikiwa na PSSSF (86%) na Jeshi la Magereza (14%) na kimeajiri watu 294. Aidha, hadi sasa Serikali imewekeza jumla ya TZS 142 bilioni.



Kwa upande wake, Mbunge Jackson Kiswaga (Kalenga) alipongeza taasisi za umma, PSSSF kwa uwekezaji mzuri kwenye kiwanda na NSSF kwa kuendesha ‘Skimu ya Hifadhi’ katika viwango vinavyokubalika.

Kwa upande wake, Mbunge Rashidi Shangazi (Mlalo) pamoja na pongezi alishauri sekta binafsi ikaribishwe katika uendeshaji wa kiwanda ili kuongeza nguvu katika masoko na uzalishaji.

Akifafanua kuhusu hoja mbalimbali za Wabunge, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo alisema kiwanda kinatoa elimu ya madhara ya uwekaji chapa mifungo na uchunaji usio bora.


“Mifugo ikiwa na chapa na ikichunwa vibaya thamani ya ngozi hupunguza kipato kwa mfugaji,” amesema Mkurugenzi Mkuu Magambo akifafanua kuhusu hatua zinazochukuliwa na kiwanda ili kupata ngozi bora.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo, akitoa mada kwa Waheshimiwa Wabunge katika semina leo tarehe 15 Juni, 2026 bungeni.

Akizungumza kuhusu ushirikiano na sekta binafsi, Bw. Magambo alisema kiwanda na PSSSF zipo tayari kufanya kazi na sekta binafsi.

“Tunawakaribisha sekta binafsi waje tushirikiane kuendesha kiwanda hiki, hivyo mwenye mawazo na uwezo wa kushirikiana nasi anakaribishwa wakati wowote,” amesema Mkurugenzi Magambo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, akitoa neno la utangulizi katika semina hiyo ya Waheshimiwa Wabunge katika Ukumbi Mdogo wa Bunge wa Pius Msekwa leo tarehe 15 Juni, 2026 Dodoma


Awali akitoa neno la utangulizi katika semina hiyo, Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu alisema lengo la kuendesha semina hiyo ni kuwajengea uelewa wabunge kuhusu fursa zilizopo KLICL na faida za ‘Skimu ya Hifadhi’.