Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF YAWANOA WAAJIRI ARUSHA KUTOKOMEZA UCHELEWESHAJI WA MAFAO YA WASTAAFU

PSSSF YAWANOA WAAJIRI ARUSHA KUTOKOMEZA UCHELEWESHAJI WA MAFAO YA WASTAAFU

News
News

Julai 2, 2026 ARUSHA


Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeendesha semina maalum kwa Maafisa Rasilimaliwatu wa mkoani Arusha, ukisisitiza ushirikiano wa karibu ili kufanikisha azma ya kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati inafanikiwa na kuondoa urasimu.

Meneja wa PSSSF Kanda ya Kaskazini Magharibi, Bw. Yessaya Mwakifulefule akitoa mada katika semina ya PSSSF kwa maafisa Rasilimaliwatu iliyofanyika leo jijini Arusha.

​Meneja wa PSSSF Kanda ya Kaskazini, Bw. Yessaya Mwakifulefule, amewataka maafisa hao kuwa kiungo muhimu kwa kuhakikisha michango ya mtumishi iko sawa katika kipindi chote cha ajira yake kabla ya kustaafu, huku akisisitiza jukumu la msingi la kuwasajili watumishi wote wapya punde tu wanaporipoti kazini ili kufanikisha kaulimbiu ya kumlipa jana mstaafu wa leo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Bw. Jacob Rombo akizungumza katika semina ya PSSSF kwa maafisa Rasilimaliwatu iliyofanyikaleo jijini Arusha.

​Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Bw. Jacob Rombo, amewataka watumishi hao kuwa na hofu ya Mungu katika kutekeleza majukumu yao na kuwasilisha maombi ya mafao kwa wakati.

Afisa Matekelezo wa PSSSF Kanda ya Kaskazini Magharibi, Bw. Venance Mwaijibe akitoa mada katika semina ya PSSSF kwa maafisa Rasilimaliwatu iliyofanyika leo jijini Arusha.

Bw. Rombo amekumbusha kuwa watendaji hao wote ni wastaafu watarajiwa, hivyo hawapaswi kuwaacha wastaafu mtaani wakilalamika wakati wanayo nafasi hivi sasa ya kukagua taarifa zao na kuziwasilisha kwa wakati ili kuwaepusha na usumbufu.

Afisa Rasilimaliwatu wa Wilaya ya Meru, Bw. Raphael Geay akichangia mada katika semina ya PSSSF kwa maafisa Rasilimaliwatu iliyofanyika leo jijini Arusha.

​Naye Bw. Avodi Lai kutoka Taasisi ya Nelson Mandela, ametoa wito kwa Maafisa Rasilimaliwatu wenzake kuhakikisha wanawasilisha nyaraka na maombi ya kustaafu miezi sita kabla ya tarehe rasmi, mara tu wanapopata tangazo la kustaafu. Hatua hizo kwa pamoja zinalenga kuleta mapinduzi kwa kuhakikisha mtumishi anapata haki yake bila kuchelewa.

Maafisa wa PSSSF katika picha ya pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Bw. Jacob baada ya semina ya PSSSF kwa maafisa Rasilimaliwatu iliyofanyika leo jijini Arusha.