Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF YASHIRIKI TAMASHA LA CRDB BUNGE BONANZA 2026, JIJINI DODOMA

PSSSF YASHIRIKI TAMASHA LA CRDB BUNGE BONANZA 2026, JIJINI DODOMA

News
News

Dodoma, Juni 20, 2026

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeungana na taasisi nyingine kushiriki tamasha la michezo ‘CRDB Bunge Boanza’ lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 20, 2026.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Dkt. Evaline Munisi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) walioshiriki katika tamasha la CRDB Bunge Bonanza kweny uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 20, 2026.


Tamasha hilo ambalo ni tukio la kila mwaka, limewashirikisha wabunge, watumishi wa bunge, wanadiplomasia, watumishi wa benki ya CRDB, taasisi za umma na binafsi na wananchi.

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Grayson Mgunda, akicheza Pool Table kwenye tamasha la CRDB Bunge Bonanza kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 20, 2026.


Lengo la tamasha hilo ni kuimarisha afya kupitia michezo, kujenga mahusiano kati ya viongozi, wadau na wananchi.

Katika tamasha hilo, washiriki walishiriki michezo mbalimbali ikiwemo, soka, netiboli, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, kufukuza kuku, kuvuta kamba na michezo ya ndani kama vile pool table.