Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
MSTAAFU AFUNGA SAFARI KUISHUKURU PSSSF KWA KULIPWA MAFAO HARAKA

MSTAAFU AFUNGA SAFARI KUISHUKURU PSSSF KWA KULIPWA MAFAO HARAKA

News
News

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Bi. Esther Riwa (mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano), ambaye amestaafu hivi karibuni, amefika kwenye banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kutoa shukrani baada ya kulipwa Mafao siku hiyo hiyo aliyostaafu ambayo ni Mei 26, 2026.

“Nimefika hapa kutoa shukurani zangu kwa kulipwa Mafao yangu tarehe hiyo hiyo niliyostaafu na nilikua naagwa, na ilikua ni siku yangu ya kuzaliwa.... cha kufurahisha siku hiyohiyo PSSSF wakanilipa Mafao yangu. Asanteni sana PSSSF," alisema Bi. Riwa.

Naibu Waziri wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Dkt. Evaline Munisi (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Hajji Khamisi, kuhusu huduma zilizokuwa zikitolewa kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yaliyofikia kilele leo Juni 23, 2026 kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Aidha Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala PSSSF, Bw. Paul Kijazi, amewahimiza wanachama wa PSSSF kutumia huduma za kiganjani kwani zinarahisisha utoaji huduma.

“Tangu Maonesho haya yaanze na leo yanafikia kilele, tumehudumia zaidi ya wanachama 460, na wengi waliunganishwa na huduma za PSSSF Portal,” alisema.

Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishiw a Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi (katikati waliosimama), akifuatilia utoaji huduma kwa wanachama unavyoendelea kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma (kulia kwake) ni Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Lulyalya Sayi.

Kwa upande wake Maneje wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Lulyalya Sayi, aliwahakikishia wanachama wa PSSSF kuendelea kupokea huduma bora na kutoa wito kwa wale wanaokaribia kustaafu kuhakikisha wanawasilisha madai yao mapema ili iwe rahisi kuyapitia na kuwalipa kwa wakati.

Mkurugenzi wa Uendeshai Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hajji Khamisi, akisalimiana na mwanachama wa PSSSF aliyefika kupata elimu kuhusu masuala ya Mafao kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma Juni 23, 2026.

“Kaulimbiu yetu hivi sasa ni tunalipa jana, kwa hivyo tunawahimiza wanachama wetu kufuatilia taarifa zao, wanapokaribia kustaafu watoe taarifa mapema kupitia PSSSF portal ili malipo yafanyike mapema,” alisisitiza Bw. Sayi.