Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF YAWAKARIBISHA WANANCHI SABASABA KUPATA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII

PSSSF YAWAKARIBISHA WANANCHI SABASABA KUPATA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII

News
News

Dar es Salaam, Juni 30, 2026


Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unashiriki Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2026, ukiahidi kutoa huduma na elimu ya hifadhi ya jamii kwa wanachama na wananchi watakaotembelea banda lake.

Mwanachama akiwa mwenye furaha wakati anapatiwa huduma kwenye banda la Mfuko wa PSSSF kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) viwanja vya Julius Nyerere Juni 30, 2026

Akizungumza katika banda la PSSSF katika maonesho hayo, Afisa Mkuu wa Uhusiano PSSSF Bi. Rehema Mkamba, amesema maonesho ya Sabasaba ni fursa muhimu ya kuwafikia wananchi wengi kwa wakati mmoja, kuwahudumia, kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi papo kwa papo pamoja na kuhamasisha matumizi ya huduma za kidijitali (PSSSF Portal) kupitia simu za kiganjani.

Mwanachama akihudumiwa kwenye banda la Mfuko wa PSSSF kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) viwanja vya Julius Nyerere Juni 30, 2026

Katika huduma za kidigitali, PSSSF inarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama na wastaafu kama vile kupata taarifa za michango, taarifa za mafao, kuwasilisha madai, kuhuisha taarifa za wategemezi, kuuliza maswali, lakini pia kwa wastaafu kuweza kujihakiki.


“Kama ambavyo kaulimbiu ya maonesho ya mwaka huu inavyosema, 'Sabasaba, Fahari ya Tanzania; PSSSF tunasema tunamuhakikishia mwanachama kesho ya uhakika kwa kuwahudumia

Wanachama.


Bi. Mkamba amesema, Wananchi watapata fursa ya kuzifikia fursa zinazotokana na uwekezaji wa Mfuko kwenye viwanda na majengo ya biashara na makazi.

Watoa huduma wa Mfuko wa PSSSF walioko kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) viwanja vya Julius Nyerere ili kuwahudumia wanachama na wananchi

“Njoo uone na ufaidike na uwekezaji wa PSSSF kwa kujipatia nyama nzuri yenye viwango vya kimataifa, bidhaa za ngozi kama vile viatu, mikoba na mikanda." Alisema Bi. Mkamba na ambaye amewakaribisha wanachama na wananchi kutembelea banda la PSSSF bila kukosa