Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF yatoa elimu kwa Makatibu wa Kamati za Bunge

PSSSF yatoa elimu kwa Makatibu wa Kamati za Bunge

News
News

*Mmoja atoa ushuhuda wa ‘Tunalipa Jana’

Morogoro, Julai 31, 2026

Watumishi wa idara ya Kamati za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameridhishwa na huduma zinatolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa watumishi wa Umma (PSSSF), wameshauri PSSSF izidishe ubunifu ili kurahisisha huduma kwa Wanachama wake.

Leo Julai 31, 2026 mjini Morogoro PSSSF ilitoa elimu ya Mfuko katika semina ya watumishi hao wa Bunge kwa lengo la kuwajenga uwelewa wa Kinga ya Jamii, "hongereni sana kwa huduma nzuri, matumizi ya kidijitali yamerahisisha sana huduma, kila kitu kinaanza na kumalizika kwenye simu au kifaa kingine chochote cha kidijitali” alisema Bi. Angelina Sanga.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji PSSSF, Bw. Hajji Moshi, akizungumza wakati wa semina maalum ya kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Makatibu wa Kamati za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanyika mjini Morogoro tarehe 31 Julai, 2026.

Aidha, wajumbe wa semina hiyo walishauri sera ya Kiga ya Jamii ipitiwe ili iweze kwenda na wakati. Mtumishi Mstasaafu wa Bunge, Bw. Gerald Magili alithibitisha kuwa PSSSF ‘inalipa jana’ kwa kusema, “nilitoa taarifa ya kuomba kibali cha kustaafu kwa mwajiri miezi sita kabla ya kusataafu, tarehe yangu ya kustaafu ilikuwa ni 25 Juni 2026, siku hiyo hiyo nilipokea mafao yangu ya kustaafu, hakika PSSSF mpo vizuri”.

Akizungumza katika semina hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSSSF, Bw. Hajji Moshi alishukuru ofisi ya Bunge kwa kutoa nafasi kwa PSSSF kufanya semina hiyo na kusema kuwa Mfuko uko tayari wakati wowote kutoa elimu ya Kinga ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Bunge na Wanachama wengine

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Kamati za Bunge, Bw. Michael Chikokoto, akizungumza wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge kwa ajili ya Makatibu wa Kamati za Bunge mjini Morogoro.

“Kwa niaba ya Menejimenti ya PSSSF, tunashukuru kupokea maoni kutoka kwenu, yote tumeyachukua na tutayafanyia kazi na yale ya Kisera tutayafikisha kwa Mamlaka husika,” alisema Bw. Moshi.

Kwa upande wake, Bw. Michael Chikokoto, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Kamatii za Bunge, alisema, “tunawashukuru PSSSF kwa kuitikia wito wetu, naamini tumejifunza mengi na tatakuwa mabalozi wenu kwa watumishi wengine wa Bunge."

Mtumishi kutoka Ofisi ya Bunge, Bi. Angelina Sanga (kushoto), akiwa na Afisa Matekelezo kutoka PSSSF, Bi. Upendo Chilewa, wakati wa semina hiyo mjini Morogoro. Bi. Sanga alipokuwa akijisajili kaaika huduma ya mifumo ya kidijitali.

Mtumishi Mstaafu wa Bunge, Bw. Gerald Magili, akitoa ushuhuda wake wakati wa semina hiyo mjini Morogoro. Bw. Magili aliipongeza PSSSF kwa kulipa mafao yake kwa wakati