Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
NAIBU WAZIRI DKT. MUNISI ASIFIA UBUNIFU BANDA LA PSSSF

NAIBU WAZIRI DKT. MUNISI ASIFIA UBUNIFU BANDA LA PSSSF

News
News

Dar es Salaam, 05/07/2026

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Dkt. Eveline Munisi, amepongeza ubunifu wa teknolojia uliofanywa na PSSSF kwa kutoa huduma kupitia meza janja.

Ametoa pongezi hizo Julai 5, 2026 alipotembelea banda la Mfuko wa PSSSF katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), na kujionea namna Mfuko unavyotoa huduma kwa wananchi kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kidijitali.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Dkt. Eveline Munisi (aliyeketi), akiwa na Kamishna wa Kazi, Bi. Suzan Mkangwa, akielezwa na Afisa Uhusiano Mfuko wa PSSSF, Bi. Jackline Jackson, jinsi wanavyohudumia wanachama kupitia Meza janja (Smart Table) kwenye banda la Mfuko, katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 5, 2026. (wapili kushoto) ni Afisa Mkuu wa Uhusiano PSSSF, Bw. Abdul Njaidi.

Katika ziara hiyo, Dkt. Munisi, ambaye aliambatana na Kamishna wa Kazi nchini, Bi. Suzan Mkangwa, alipokelewa na Afisa Mkuu wa Uhusiano wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi, aliyempa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko pamoja na maboresho yaliyofanyika katika kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama na wananchi.


“ Hongereni sana PSSSF kwa kutoa huduma kidijitali na kisasa zaidi, ubunifu huu unavutia zaidi na kurahisisha huduma kwa wateja.” Alipongeza.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Dkt. Eveline Munisi (wa pili kulia) na Kamishna wa Kazi Bi. Suzan Mkangwa (wa pili kushoto), wakiangalia ubora wa mikoba ya kike inayotengenezwa kwenye kiwanda cha Bidhaa za Ngozi Kilimanjaro (KLICL), katika banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 5, 2026.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano (Mhe. Eveline Munisi (kushoto), akipatiwa maelezo na kiongozi wa Masoko na Mauzo, Machinjio ya Nguru Hills Ranch, Bw. Seth Thomas, alipotembelea banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 5, 2026.

Akiwa katika banda la ushirikiano la PSSSF na NSSF, Naibu Waziri alitembelea eneo la utoaji huduma na kushuhudia namna wananchi wanavyohudumiwa kwa ufanisi. Aidha, alipata fursa ya kutembelea sehemu ya maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi (KLICL) pamoja na nyama inayozalishwa katika Machinjio ya Nguru Hills, miongoni mwa uwekezaji uliofanywa na PSSSF kwa kushirikiana na wabia wengine.