Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
KATIBU MKUU MKOMI AIPONGEZA PSSSF MAONESHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

KATIBU MKUU MKOMI AIPONGEZA PSSSF MAONESHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

News
News

Na Mwandishi wetu, Dodoma


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi, Bw. Juma Mkomi, ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kushiriki na kutoa huduma katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma Juni 22, 2026.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumsihi, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akifurahia jambo baada ya Meneja Rasilimaliwatu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Gloria Mboya (katikati mwenye fulana nyeusi) kumpatia maelezo ya huduma zinazotolewa kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma Juni 22, 2026.


“Niwapongeze sana kwa ushiriki wenu, lakini pia kwa kutoa elimu na kuhudumia wananchi, naamini katika maonesho haya mmekutana na wanachama wenu wengi, hongereni sana," alisema Bw. Mkomi.


"Hadi kufikia leo alasiri Juni 22, 2026, jumla ya wananchi 365 walitembelea kwenye banda letu, na tumewahudumia vizuri, wengi wao wameunganishwa na huduma za kidijitali (PSSSF Portal)," alisema Meneja Rasilimaliwatu PSSSF Bi. Gloria Mboya wakati akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Mkomi.

Wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), wakiunganishwa kutumia PSSSF Portal kupitia simu zao za mkononi, walipotembela banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. Kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa wanachama wa Mfuko waliotembea banda la PSSSF.


Kwa kutumia simu janja au kompyuta wanachama anaweza kuongia kwenye PSSSF Portal kuangalia michango yake, kuwasilisha madai mbalimbali na kufatilia, kuhuwisha taarifa zake na za wategemezi wake, na kwa wastaafu wanaweza kujihakiki.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumsihi, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akipokea zawadi ya machapisho yenye taarifa za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kutoka kwa Meneja Rasilimaliwatu PSSSF, Bi. Gloria Mboya kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma Juni 22, 2026.


Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyobeba kaulimbiu isemayo 'Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu' yanatarajiwa kufikia kilele Juni 23, 2026.