Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF IMEYAFANYA MAISHA KUWA RAHISI -WANACHAMA

PSSSF IMEYAFANYA MAISHA KUWA RAHISI -WANACHAMA

News
News

Dodoma, Juni 19, 2026

Maboresho yaliyofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kupata huduma kupitia PSSSF Kidijitali yameleta urahisi kwa wanachama wa Mfuko huo, hayo yamebainishwa na wanachama wa Mfuko waliotembelea kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Afisa Utumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TARIRI), Bi. Odilia Marenga, akiwa kwenye banda la PSSSF Juni 18, 2026

Afisa Utumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TARIRI), Bi. Odilia Marenga.

amebainisha alipotembelea banda la huduma la PSSSF katika viwanja hivyo amesema watumishi wa TARIRI walionufaika na mafao kutoka PSSSF ni shuhuda, wamekuwa wakipiga simu kueleza furaha yao kwa jinsi walivyopokea mafao haraka.

“Tangu huduma zianze kutolewa kupitia PSSSF portal, zimekuwa zikitolewa kwa wakati, tofauti na hapo nyuma.... hali hii imekuwa ikiwafurahisha wastaafu wetu na wale akina mama wanaoomba fao la uzazi,” alisema Marenga.

Afisa Utumishi PSSSF, Bw. Denis Kaitwa, (kulia), akimuunganisha mwanachama wa PSSSF, Bi. Rebeca Hoza na huduma ya PSSSF Kidijitali kupitia simu janja, alipotembelea banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Utu,kishi wa Umma Kitaifa kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma Juni 17, 2026

Naye Bi. Rebeca Hoza, ambaye ni mwanachama wa PSSSF, yeye amesifu huduma ya PSSSF Kidijitali, amekuwa akipata huduma kupitia kiganjani, “nikitaka kuangalia michango yangu au taarifa zozote, sihangaiki tena, PSSSF wamefanya maisha yetu kuwa rahisi.”

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano Bw. Revocatus Kasimba (katikati), akielekezwa namna ya kujiunga na PSSSF Portal na Afisa Mkuu wa Uhusiano, Bw. Abdul Njaidi (kulia na Afisa Mafao Mwandamizi PSSSF, Bi. Roselyne Tineishemo kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Kitaifa kwenye vuiwanja vya Chinangali jijini Dodoma Juni 19, 2026

Akizunguma kuhusu mafanikio hayo ya utoaji huduma, Kaimu Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati- Dodoma, Bi. Jane Mbuya amewashukuru wanachama wa PSSSF kwa kuonyesha ushirikiano kwa kutumia huduma hiyo ya PSSSF portal.

Timu ya PSSSF katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo Juni 19, 2026

“Ushuhuda ni kwamba hata ukipita kwenye ofisi zetu hutakuta foleni za wanachama wakipata huduma, kwani tumesogeza huduma kupitia PSSSF Kidijitali hii imeturahisishia, sasa hivi tunachakata mafao ya mstaafu kabla hajaondoka ofisini, akistaafu na mafao yake yako tayari, hii ni kutokana na kutumia mifumo kutoa huduma," alisisitiza Bi. Mbuya.