Mradi wa PSSSF Olorien ni Mfano, sasa unavuna faida
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kusimamia vyema mradi wa nyumba za makazi wa Oloirieni uliopo jijini Arusha ambao unaendelea kuvuna faida kwa PSSSF na kuufanya Mfuko uweze kutekeleza vyema majukumu yake.
Kauli hiyo imetolewa jijini Arusha na mwenyekiti wa PIC, Mhe. Augustine Vuma Holle wakati wa kikao cha majumuisho baada ya kamati hiyo kutembelea mradi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru akitoa taarifa ya utekelezaji mbele ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ilipotembelea mradi wa nyumba za makazi wa Oloirieni uliopo jijini Arusha unaomilikiwa na PSSSF.
“Kamati imeridhishwa na mradi huu, mradi huu ni mradi wa mfano, hili ni jambo jingine uwekezaji mkubwa na wa kisasa, hakika eneo hili kwa ubora wake linatuaheshimisha kama taifa. Pia kamati inaelekeza kuwe kunafanyika ukarabati wa mara kwa mara kwenye mradi huu na PSSSF ifatilie wadaiwa sugu” alisema Mwenyekiti huyo wa PIC.
Kwa upande wake makamu Mwenyekiyi wa kamati hiyo, Mhe. Mary Masanja alisema, “Kazi nzui inaonekana wazi,kubwa ambalo mimi nimeliona ni jinsi mradi huu ulivyotoa fursa kwa watu mbalimbali kufanyakazi ambazo zinawaingizia kipato, hongereni sana”.