Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo

Sickness Benefit

Mafao ya ugonjwa yanatolewa kwa mujibu wa Ibaya ya 29 ya Sheria Namba 2 ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ya Mwaka 2018.


Ikitokea mwanachama ameugua muda mrefu, kwa mujibu wa Sheria za Kazi, hulipwa mshahara kamili kwa muda wa miezi mitatu. Miezi mitatu inayofuata atalipwa nusu ya mshahara wake, baada ya hapo ajira itakoma.

Masharti ya Ulipaji wa Mafao ya Ugonjwa

  • Awe Mwanachama wa PSSSF,
  • Awe amechangia kwa kipindi cha miezi 36, ambapo miezi 12 kati ya hiyo iwe imelipwa ndani ya mwaka mmoja kabla ya ugonjwa,
  • Awe hajatimiza umri wa kustaafu kwa hiari.
  • Awe anaumwa au amepata ajali ambayo haijatokana na kazi yake na atalipwa asilimia arobaini (40%) ya mshahara aliokuwa akipata kabla ya ugonjwa au ajali. Mafao haya yatalipwa kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu.

Nyaraka zinazohitajika: -

  • Fomu namba PS-BEN.4,
  • Uthibitisho wa Uraia wa Tanzania (Cheti cha Kuzaliwa, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya Kusafiria, Kitambulisho cha Mpiga Kura),
  • Taarifa ya likizo ya ugonjwa kutoka kwa mwajiri (baada ya siku 63 za likizo ya ugonjwa kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini),
  • Taarifa ya taratibu za matibabu,
  • Nakala ya kadi ya benki,
  • Taarifa ya benki,
  • Nakala ya hati ya kupokelea mshahara