Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
WAKURUGENZI PSSSF WATOA HUDUMA KWA WANACHAMA NA WANANCHI MAONESHO YA NANENANE DODOMA

WAKURUGENZI PSSSF WATOA HUDUMA KWA WANACHAMA NA WANANCHI MAONESHO YA NANENANE DODOMA

News
News

Dodoma, Agosti 6, 2026

Wakurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wameungana na watumishi wengine wa Mfuko kutoa huduma kwa wanachama na wananchi wanaotembelea Banda la PSSSF katika Maonesho ya Kilimo na Uvuvi (Nanenane) yanayofanyika kitaifa kwenye Viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.

Huduma zinazotolewa katika banda la PSSSF ni pamoja na elimu kuhusu hifadhi ya jamii, kuwaunganisha wanachama na wastaafu kwenye huduma za kidijitali kupitia PSSSF Kiganjani na PSSSF Portal, pamoja na kutoa taarifa kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana kupitia miradi ya Mfuko, ikiwemo Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha KLICL na Machinjio ya Kisasa ya Nguru Hills yaliyopo wilayani Mvomero.

Mkurugenzi wa TEHAMA, Mfuko wa PSSSF, Bw. Eric Kato, akimuhudumia mwanachama, Agosti 5, 2026

Wakurugenzi waliotoa huduma Agosti 6, 2026 ni Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Bw. Paul Kijazi; Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Hilda Nkunna; na Mkurugenzi wa Manunuzi na Ugavi, Bw. Jimmy Mbogela.

Awali, Agosti 5, 2026, Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Eric Kato, aliungana na watumishi wa Mfuko kutoa huduma kwa wanachama na wananchi waliotembelea banda hilo. Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Hajj Moshi, aliongoza timu ya wataalamu wa PSSSF kutembelea mabanda mbalimbali ya waoneshaji ili kutoa elimu kuhusu maboresho ya huduma za Mfuko na kupokea maoni kutoka kwa wanachama na wananchi.

Kwa mujibu wa Meneja wa Uhusiano na Elimu kwa Wanachama wa PSSSF, Bw. Omega Ngole, ushiriki wa wakurugenzi katika utoaji wa huduma unaonesha dhamira ya uongozi wa Mfuko ya kuwathamini wanachama na wananchi, huku ukiwapa motisha watumishi kuendelea kutoa huduma bora zenye weledi na ufanisi.

"Ushiriki wa wakurugenzi katika kuhudumia wanachama ni sehemu ya utamaduni wa PSSSF wa kusogeza huduma karibu na wananchi na kuhakikisha kila mteja anapata huduma bora kwa wakati," alisema Bw. Ngole.

Wakurugenzi wa PSSSF , wakitembelea mabanda ya wadau wa Mfuko kwenye Maonesho ya Kilimo na Uvuvi (Nanenane) Viwanja vya Dkt. John Malecela eneo la Nzuguni jijini Dodoma, Agosti 6, 2026

Aliongeza kuwa, mbali na maonesho ya kitaifa yanayofanyika Dodoma, PSSSF pia inatoa huduma katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye kanda nyingine nchini, ambazo ni Kanda ya Magharibi mkoani Tabora, Kanda ya Ziwa Magharibi jijini Mwanza, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya, Kanda ya Kusini katika Manispaa ya Lindi, pamoja na Zanzibar.

Wakurugenzi wa PSSSF kutoka kushoto, Mkurugenzi wa Manunuzi na Ugavi Bw. Jimmy Mbogela, Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utuwala, Bw. Paul Kijazi na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Hilda Nkunna, wakitembelea mabanda ya wadau wa Mfuko kwenye Maonesho ya Kilimo na Uvuvi (Nanenane) Viwanja vya Dkt. John Malecela eneo la Nzuguni jijini Dodoma, Agosti 6, 2026