Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF YAFANYA ZIARA KATIKA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM

PSSSF YAFANYA ZIARA KATIKA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM

News
News

Septemba 11, 2026


Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ulifanya ziara ya kimkakati katika vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam. Ziara hii ililenga kujenga na kuimarisha uhusiano wa kikazi pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Mfuko na vyombo hivyo katika kutoa elimu kwa wanachama na wananchi kwa ujumla.

Mhariri wa habari gazeti la Mwananchi katika Kampuni ya Mwananchi, Bw. Noor Shija aklitoa maelezo jinsi ofisi inavyofanya kazi kwa maafisa wa PSSSF katika ziara hiyo.


Katika ziara hiyo, ujumbe wa PSSSF ulifanikiwa kutembelea kituo cha redio cha Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam cha City FM, Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi, Kituo cha Redio cha Uhuru FM pamoja na Umoja wa Mtandao wa Wanablogu Tanzania.


Ujumbe huo uliongozwa na Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko, Bw. Abdul Njaidi, alieleza kuwa ushirikiano huo utakuwa jukwaa muhimu litakalosaidia kufikisha taarifa za huduma mbalimbali za Mfuko kwa jamii kwa urahisi zaidi.

Bw. Njaidi alisisitiza kuwa PSSSF inaamini kupitia vyombo hivyo vya habari jamii itapata uelewa mpana wa jinsi Mfuko unavyofanya kazi na kutoa huduma zake.

Afisa Uhusiano na Elimu kwa Wanachama wa PSSSF Bw. Abdul Njaid pichani akiwa na Bw. Mkula Kitambi Mhasibu mkuu na meneja Utawala na Sam Maitarya Meneja Biashara katila ziara ya PSSSF kutembelea kituo cha redio cha Uhuru FM, Jijini la Dar es Salaam.


Pia alitumia fursa hiyo kukumbusha na kujivunia kauli mbiu ya Mfuko ya 'Tunalipa Jana', ikiwa ni ishara ya msisitizo na utayari wa kuwahudumia wanachama na kulipa stahiki zao kwa wakati.

Kwa upande wao, viongozi wa vyombo hivyo walipokea ujio wa PSSSF vizuri na kuahidi ushirikiano wa karibu.

Afisa Uhusiano na Elimu kwa Wanachama wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi, akimkabidhi jarida PSSSF Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN), Bw. Beda Msimbe, wakati wa ziara ya PSSSF katika ofisi za TBN, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. ​Wengine pichani ni watumishi wa PSSSF na viongozi wa TBN.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Tabu Shaibu, alithibitisha utayari wa City FM kushirikiana na Mfuko, huku Mwandishi na Mdhamini wa Umoja wa Mtandao wa Wanablogu, Bw. Issa Michuzi, akipongeza hatua hiyo na kuahidi kutumia blogu takriban mia mbili zilizoko chini ya umoja huo kuelimisha umma.