Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
PSSSF YATWAA TUZO YA MSHINDI WA KWANZA UTAYARISHAJI TAARIFA ZA FEDHA 2025/26

PSSSF YATWAA TUZO YA MSHINDI WA KWANZA UTAYARISHAJI TAARIFA ZA FEDHA 2025/26

News
News

Dar es Salaam, Novemba 26, 2026

Na Mwandishi wetu,

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetwaa Tuzo ya Mshindi wa Kwanza ya Utayarishaji na Uwasilishaji Taarifa za Fedha kwa kuzingatia viwango vya kitaaluma vya kimataifa mwaka wa fedha 2025/26 (Best Presented Financial Statements) kundi la Taasisi za Hifadhi ya Jamii.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua (kushoto), akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Ali Yakiti, baada ya Mfuko huo kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za umma zinazotoa huduma za hifadhi ya jamii, kwa umahiri katika utayarishaji na uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa kuzingatia ubora wa kimataifa mwaka 2025/26. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo imefanyika katika Hoteli ya APC, Bunju, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Novemba 27, 2026. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA. Profesa Siasa Mzenzi.

Mkurugenzi wa Fedha Mfuko wa PSSSF Bw. Ally Yakiti alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mfuko kutoka kwa mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Nsubili Joshua katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya APC Bunju, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Novemba 27, 2026.

Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mfuko huo kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za umma zinazotoa huduma za hifadhi ya jamii, katika tuzo za umahiri wa utayarishaji na uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa kuzingatia viwango vya kimataifa kwa mwaka 2025/26.

Tuzo ya mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za umma zinazotoa huduma za hifadhi ya jamii, kwa umahiri katika utayarishaji na uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa kuzingatia ubora wa kimataifa mwaka 2025/26.

Tuzo hizo hutolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kila mwaka ili kushajihisha umahiri katika utayarishaji na uwasilishaji wa taarifa za fedha.