PSSSF YAPEWA TUZO YA SHUKRANI JUKWAA LA C-CEOs 2026
Arusha, Septemba 30, 2026
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepewa Tuzo ya Shukrani kwa kutambuliwa miongoni mwa taasisi zilizowezesha kufanyika kwa Jukwaa la Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (C-CEOs Forum) 2026.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka (kulia) akiwa katika picha na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Dkt. Irene Isaka, baada ya kumkabidhi cheti cha shukrani kwa niaba ya PSSSF kwa miongoni mwa taasisi zilizowezesha kufanyika kwa Jukwaa la C-Ceos 2026, wakati wa hafla ya kufunga jukwaa hilo lililofanyika kwa sikutatu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha, AICC Septemba 30, 2026
Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga Jukwaa hilo iliyofanyika Septemba 30, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha.

Mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa jukwaa hilo la C-CEOs 2026
Balozi Dkt. Kusiluka alimkabidhi tuzo hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF, Dkt. Irene Isaka, kwa niaba ya Mfuko. Jukwaa la C-CEOs Forum 2026 limewakutanisha Wenyeviti wa Bodi, Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, viongozi wa Serikali, washirika wa maendeleo, wawekezaji, wadhibiti pamoja na wadau wengine, kwa lengo la kujadili masuala ya kimkakati yanayohusu ufanisi wa Taasisi za Umma na mchango wake katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Watumishi wa PSSSF wakiwa na cheti hicho kwenye banda la kutoa elimu na hudumakwa wanachama wa Mfuko kwenye viwanja vya kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC jijini arusha Septemba 30, 2026.