Coat of Arms

PUBLIC SERVICE SOCIAL SECURITY FUND

Leo. Kesho. Pamoja.

PSSSF Logo
WASHIRIKI 460 WA MKUTANO WA ALAT WANUFAIKA NA ELIMU YA PSSSF

WASHIRIKI 460 WA MKUTANO WA ALAT WANUFAIKA NA ELIMU YA PSSSF

News
News

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Washiriki 460 wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), ambapo wengi wao ni wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), wamepata fursa ya kunufaika na elimu kuhusu huduuma zitolewazwo na Mfuko huo, maboresho yaliyofanyika katika huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wanachama na wastaafu.

Elimu hiyo ilitolewa kwa washiriki na Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Mfuko wa PSSSF, CPA Rajabu Kinande katika Mkutano na kupitia banda lake katika maonesho yaliyoambatana na mkutano huo uliofanyika kuanzia Novemba 16 hadi 19, 2026, jijini Mwanza.

Meneja wa PSSSF kanda ya Ziwa Mashariki CPA. Rajabu Kinande akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo Bi. Dotto Elias kisharika, Mtendaji wa kijiji wakati wa maonyesho yaliyokuwa yakiendelea sambamba na Mkutano Mkuu wa ALAT jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano, CPA Rajabu Kinande, amesema ushiriki wa Mfuko katika mkutano huo umekuwa fursa muhimu ya kuwafikia wanachama na wadau wengine kwa kuwapatia taarifa sahihi kuhusu majukumu ya PSSSF na maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika mifumo na sheria zinazosimamia shughuli za Mfuko.

Watumishi wa Mfuko wa PSSSF wakionyeshana namna tehama inavyorahisisha huduma ya madai ya Mafao katika Mfuko huo na kwa wanachama wake

Amesema kupitia mkutano huo, PSSSF imeweza kuwaelimisha washiriki kuhusu maboresho ya mafao yanayotolewa na Mfuko pamoja na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika kuboresha utoaji wa huduma.

“Tumefanikiwa kuwajulisha wanachama wetu kuhusu maboresho ya mafao yanayotolewa na Mfuko, pamoja na matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma. Hatua hizi zinalenga kuhakikisha wanachama na wastaafu wanapata huduma bora, kwa urahisi na kwa wakati chini ya kaulimbiu yetu ya tunalipa jana,” amesema CPA Kinande.

Afisa Mauzo KLICL Bw. Christopher Mbonyani akimuhumia Mteja katika maonyesho yanayoendelea sambamba na mkutano Mkuu wa ALAT, Leo 17 Novemba, 2026 Mwanza.

Ameongeza kuwa PSSSF itaendelea kutumia majukwaa mbalimbali ya mikutano na maonesho kuwafikia wanachama na wadau wake ili kuongeza uelewa kuhusu masuala ya hifadhi ya jamii na huduma zinazotolewa na Mfuko.

Afisa Matekele PSSSF kanda ya Ziwa Mashariki, Bw. Saidi Kipindura, akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo, Bw.Exavery Ntambala Balikenye DED Kigoma, jinsi ya kuomba Mafao kupitia tehama