SANGU AIPONGEZA PSSSF: “MNAFANYA KAZI NZURI SANA, ENDELEENI HIVYO HIVYO”
Sumbawanga, Oktoba 14, 2026
Na Mwandishi Wetu, Sumbawanga
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa juhudi zinazofanywa katika kuboresha huduma na kuhakikisha wanachama na wastaafu wanapata mafao yao kwa wakati.

Picha ya pili: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la PSSSF katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Mhe. Sangu ametoa pongezi hizo Oktoba 13, 2026, alipotembelea banda la PSSSF katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa, yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa. Maonesho hayo yanafikia kilele leo, Oktoba 14, 2026.

Mwanachama wa PSSSF akipatiwa huduma na mtumishi wa Mfuko huo katika banda la PSSSF wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
“Hongereni, mnafanya kazi nzuri sana, endeleeni hivyo hivyo. Kabla ya kuja hapa, nilifungua semina ya wastaafu watarajiwa wa PSSSF na kuwaeleza kuwa chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mfuko umeimarika na unaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, ikiwemo kulipa mafao kwa wakati. Hivyo, endeleeni kufanya kazi nzuri ili wastaafu wetu waendelee kufurahia huduma za Mfuko wao,” alisema Mhe. Sangu.

Mwanachama wa PSSSF akipatiwa huduma na mtumishi wa Mfuko huo katika banda la PSSSF wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Aidha, Mhe. Sangu alielezwa kuwa PSSSF inashiriki maonesho hayo kwa lengo la kuwafikia wanachama na wananchi kwa ujumla, kutoa elimu kuhusu hifadhi ya jamii na kuwahudumia wanachama, wakiwemo wastaafu.
Kupitia maonesho hayo, PSSSF inaendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii, maandalizi ya kustaafu na huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko. Vilevile, maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kufahamu maboresho yaliyofanyika katika mifumo ya utoaji huduma na mafao, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama.

Mwanachama wa PSSSF (kulia), akipatiwa huduma na mtumishi wa Mfuko huo katika banda la PSSSF wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.