MWENYEKITI WA BODI NA MKURUGENZI MKUU WA PSSSF WASHIRIKI C-CEOs FORUM 2026
Arusha, Septemba 28, 2026
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Dkt. Irene Isaka, na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko, Bw. Fortunatus Magambo, wameshiriki katika Jukwaa la C-CEOs Forum 2026, lililofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha, Septemba 28, 2026.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Fortunatus Magambo akiwa na viongozi wengine kwenye Jukwaa la C-CEOs Forum 2026, lililofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha, Septemba 28, 2026.
Jukwaa hilo limefanyika chini ya kaulimbiu “Mashirika ya Umma Yenye Ufanisi wa Juu kwa Ajili ya Uchumi Shindani, Jumuishi na Himilivu: Kuelekea Utekelezaji wa Dira 2050.”
Ushiriki wa PSSSF katika jukwaa hilo unalenga kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kimkakati na wadau mbalimbali, pamoja na kutoa fursa kwa viongozi wa taasisi za umma kubadilishana uzoefu na kujadili mikakati ya kuongeza ufanisi, ubunifu na ushindani katika utendaji wa taasisi za umma, sambamba na kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Dkt. Irene Isaka kwenye Jukwaa la C-CEOs Forum 2026, lililofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha, Septemba 28, 2026.
Aidha, PSSSF imeshiriki katika jukwaa hilo kwa kuweka banda maalum la kutoa elimu kuhusu Hifadhi ya Jamii, pamoja na kutoa huduma kwa wanachama na wastaafu wa Mfuko wanaoshiriki katika mkutano huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Fortunatus Magambo akisalimiana na viongozi mbalimbali kwenye Jukwaa la C-CEOs Forum 2026, lililofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha, Septemba 28, 2026.
Kupitia banda hilo, washiriki wanapata fursa ya kupata elimu na ufafanuzi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na PSSSF, pamoja na mifumo ya kidijitali inayowezesha wanachama kupata huduma za Mfuko kwa urahisi na kwa wakati.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Dkt. Irene Isaka (katikati) akiwa na watumishi wa PSSSF kwenye banda la Mfuko pembezoni mwa Jukwaa la C-CEOs Forum 2026, lililofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha, Septemba 28, 2026.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Fortunatus Magambo (katikati) akiwa na watumishi wa PSSSF kwenye banda la Mfuko pembezoni mwa Jukwaa la C-CEOs Forum 2026, lililofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha, Septemba 28, 2026.