WAZIRI SANGU APONGEZA THAMANI YA PSSSF KUFIKIA TRILIONI 12.55

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu akipokea zawadi ya kumbukumbu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Fortunatus Magambo alipotembelea na kukutana na Menejimenti na watumishi wa Mfuko leo Disemba 11, 2026.
Dodoma, Disemba 11, 2026
*PSSSF: Tutaendelea kutimiza majukumu yetu vizuri
Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu imeupongeza Mfuko kwa kufikia thamani ya Tsh 12.55 trilioni kutoka Tsh 5.61 trilioni wakati mifuko minne inaungana mwaka 2018.
Mhe. Sangu alitoa pongezi hizo Disemba 11, 2025 alipofanya ziara ya kikazi ya na kupokea taarifa ya utendaji wa PSSSF tangu kuteuliwa kwake kuongoza Wizara hiyo inayosimamia Kinga ya Jamii ikiwemo PSSSF.

icha ya pamoja Waziri wa NchI Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Rahma Kisuo, Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Bw. Festo Fute Menejimenti pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mfuko.
“Napongeza kukua kwa thamani ya Mfuko iliyofikia ya trilioni 12.55 kutoka trilioni 5.61 wakati mifuko ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF inaungana na kuunda PSSSF mwaka 2018 … hakika hatua hii ni kubwa mno na inatoa matumaini kwa wanachama wenu,” alisema Mhe. Waziri.

Baadhi ya Wakurugenzi wa PSSSF wakimsikiliza Mhe. Waziri Deus Sangu akizungumza.
Mhe. Waziri aliitaka PSSSF kuendelea kulipa mafao kwa wakati na kuongeza, “Kabla ya kujiunga Wizara hii, nilikuwa Wizara ya Utumishi ninajua jinsi PSSSF mnavyolipa mafao kwa wakati. Hongereni sana na endeleeni kuwalipa wastaafu mafao yao kwa wakati,” alisisita Mhe. Sangu.

Waziri wa NchI Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu akizungumza.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Riadh Kisuo, aliishauri PSSSF kuendelea kutoa elimu juu ya huduma zake ili wanachama wazijue vyema, kwani lengo la serikali inataka kila mstaafu apate haki yake kwa wakati na usahihi.

Naibu Waziri wa NchI Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano , Mhe. Rahma Kisuo
Naye Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo alimshukuru Mhe. Waziri Sangu kwa kukutana na Menejimenti na watumishi wa PSSSF.
“PSSSF tunaahidi kuendelea kutimiza majukumu yetu kwa uadilifu huku tukizingatia miongozo yote ya Serikali, tutahakikisha tunaendelea kulipa wastaafu wetu kwa wakati sahihi,” alisema Bw. Magambo.
