
NIKIWA NA SIMU YANGU NIKO NA PSSSF
Mwanachama wa PSSSF, Hawa Hamad, akionesha kwa furaha ukurasa wa PSSSF kiganjani kwake mara baada ya kuelekezwa jinsi ya kujiunga na PSSSF Kidijitali leo kwenye maonesho ya 12 ya Biashara na Utalii Tanga, yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwahako
Na Mwandishi Wetu, Tanga
“Nikiwa na simu yangu niko na PSSSF,” hayo ni maneno ya mwanachama wa PSSSF Bi. Hawa Hamad wa jijini Tanga muda mfupi baada ya kujiunga na PSSSF Kidijitali na kuanza kujihudumia yeye mwenyewe.
Afisa Matekelezo Mwandamizi PSSSF, Frederick Paschal (kushoto), akimuelekeza mwanachama wa PSSSF, Hawa Hamad, jinsi ya kujiunga na PSSSF Kidijitali leo kwenye maonesho ya 12 ya Biashara na Utalii Tanga, yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwahako
Bi. Hawa mbaye ni mtumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) jijini Tanga, ameyasema hayo Juni 4, 2025 kwenye maonesho ya 12 ya biashara na utalii Tanga, yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako.
Maofisa wa PSSSF wamefanya huduma ya kutembelea banda kwa banda kujua changamoto zao, kutoa huduma mbalimbali na kutoa elimu ya Mfuko “PSSSF Banda kwa banda” leongo ikiwa ni kuwafikishia huduma wanachama wake kwenye maonesho mbalimbali yanayozikutanisha taasisi za umma na wananchi.
Mwanachama mwingine aliyefurahishwa na huduma ya PSSSF kidijitali baada ya kujiunga ni Bw. Rutta Kihama, amesema kupitia PSSSF Kidijitali ofisi imehamia mkononi mwake.