• Call Free: 0800 110040
  • Portal Admin Form
 
  • Change Language: SW
 
  • Enquiries
  • FAQs
  • Home
  • About PSSSF
    • About Us
    • Organisation Offices
    • Board of Trustees
    • Management
  • Benefits
    • Retirement Benefit
    • Death Benefit
    • Survivor Benefit
    • Maternity Benefit
    • Unemployment Benefit
    • Sickness Benefit
    • Invalidity Benefit
  • Media Center
    • News
    • Publications
    • Photo Album
    • Video
  • Self Service
    • Member Portal
    • Billing Portal
    • QR-Codes
    • Portal Admin Form
  • Investments
    • Real Estate
    • Industial Investment
  • Tenders
    • General Procurement Notice
    • Awarded
    • Current Tender
  • e- Mrejesho
 
  Home   |   News Board
author image

PSSSF

To provide high quality social security services using competent, motivated staff and appropriate technology.

Benefit Types

  • Retirement Benefit
  • Death Benefit
  • Survivour Benefit
  • Maternity Benefit
  • Unemployment Benefit
  • Sickness Benefit
  • Invalidy Benefit

Online Services

  • Member Portal
  • Billing Portal
  • QR-Codes
ELIMU YA PSSSF KIGANJANI YAWAFIKIA WANACHAMA MAONESHO YA OSHA
2024-04-25 00:00:00

Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kaskazini, Vonness Koka (Wanne kushoto) akiwaeleza namna ya kutumia Muongozo wa wanachama wa PSSSF, wakati yeye na timu ya watumishi wa Mfuko huo kutembelea mambanda ya maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, kwenye viwanja vya General Tyre, Njiro, jijini Arusha Aprili 25, 2024. Lengo ni kuwapa elimu kuhusu matumizi ya PSSSF Kiganjani. Watatu kushoto ni Afisa Mkuu wa Uhusiano PSSSF, Abdul Njaidi

Na Mwandishi wetu, Arusha
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umewakumbusha wanachama wake kuwa, huduma zote zinazohusiana na uanachama wa mwanachama zinapatikana mtandaoni, (PSSSF Kiganjani).
Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kaskazini, Bi. Vonness Koka, amesema hayo wakati akiongoza timu ya watumishi wa Mfuko huo kupeleka elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani kwenye mabanda ya maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), kwenye viwanja vya General Tyre jijini Arusha Aprili 25, 2025.

Wafanyakazi wa CRDB wakiunganishwa kwenye PSSSF Kiganjani kutoka kwa maafisa wa PSSSF, Bi Vonnes Kosa (wapili kutoka kulia) na Bw. Venance Mwaijibe (wa kwanza kulia) wakati wa maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, kwenye viwanja vya General Tyre, Njiro, jijini Arusha Aprili 25, 2024


“Tumeanzisha mfumo wa PSSSF Kiganjani unaomuwezesha mwanachama kupata taarifa za Michango yake mahali popote alipo bila ya kufika kwenye ofisi zetu, vile vile mfumo unamuwezesha mstaafu kujihakiki akiwa nyumbani kwake, safarini au mahali popote. Tunawakaribisha wanachama wote waliopo Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Arusha na wananchi kwa ujumla, kufika kwenye banda letu ili kupata elimu hiyo ya matumizi ya PSSSF Kiganjani.” Amefafanua Bi. Koka

Timu ya PSSSF iliyoko maonesho ya OSHA, jijini Arusha tayari kuwahudumia Wanachama na wananchi wote

Amesema, kupitia simu janja, mwanachama anachohitajika kufanya ni kupakua Application ya PSSSF Kiganjani kisha atafuata maelekezo ya namna ya kujisajili na hapo ataanza kufaidi huduma hiyo ya kisasa, amesema.


Aidha Bi. Koka amesema katika maonesho hayo pia wamekuwa wakipita kwenye mabanda na kukutana na wanachama wao lengo likiwa ni kutoa elimu hiyo ya matumizi ya PSSSF Kiganjani.
“Faida ya matumizi ya PSSSF Kiganjani, licha ya kuokoa muda, lakini pia inaondoa gharama kwa mwanachama kusafiri kufuata huduma. Pia kwa upande wa Mfuko, umepunguza gharama kwa kuachana na matumizi ya karatasi kuchapisha taarifa za wanachama wanaozihitaji.” Amesema.


Wanachama nao wameeleza faida ya huduma ya PSSSF Kiganjani.

Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kaskazini, Vonness Koka (kushoto), akiwa kwenye banda la JKCI.

Mwanachama wa PSSSF, Bw. Fabian Ndokoma

“Nimefurahi sana kujua huduma ya PSSSF Kiganjani, lengo la kuja hapa kwenye banda la PSSSF, ni kupata taarifa za michango yangu, lakini wamenielekeza njia hii ya kutumia PSSSF Kiganjani kupitia simu yangu, nimepakua application yao na nimefanikiwa kuona taarifa zangu.” Amesema mwanachama wa PSSSF, Bw. Fabian Ndokoma.


Naye Bi. Esther Mlay, ambaye naye ni mwnaachama wa PSSF amesema yeye hana haja tena ya kwenda ofisi za PSSSF, tayari alikuwa amejiunga na PSSSF Kiganjani na amekuwa akifaidi huduma mbalimbali ikiwemo kuona mwenendo wa michango yake.


MWISHO.




About PSSSF

The main purpose is to collect contributions and payment of terminal benefits to employees of public service.The act shall apply in mainland Tanzania.


READ MORE

Quick Links

  • Billing Portal
  • Member Portal
  • Employer Portal
  • Announced Tenders

Get In touch

  • PSSSF House HQ , Makole, Dodoma
  • P.O.BOX 1501
  • info@psssf.go.tz
  • 0800 110040
  • Mon - Fri 8.00 - 17.00. Sat,Sun CLOSED

Zonal Offices

  • Dodoma: +255 26 2323338
  • Ilala: +255 22 2120912
  • Kinondoni: +255 22 2123848
  • Temeke: +255 22 2861039
  • Mwanza: +255 28 2506114
  • Mbeya: +255 25 2502243
  • Arusha: +255 27 2970284
  • Morogoro: +255 23 2934188
  • Mtwara: +255 23 2334661
  • Geita: +255 28 2520470
Copyright © 2024 psssf. All rights reserved.
  • Contact Us
  • Privacy Policy
  • Services
  • Disclaimer