• Call Free: 0800 110040
  • Portal Admin Form
 
  • Change Language: SW
 
  • Enquiries
  • FAQs
  • Home
  • About PSSSF
    • About Us
    • Organisation Offices
    • Board of Trustees
    • Management
  • Benefits
    • Retirement Benefit
    • Death Benefit
    • Survivor Benefit
    • Maternity Benefit
    • Unemployment Benefit
    • Sickness Benefit
    • Invalidity Benefit
  • Media Center
    • News
    • Publications
    • Photo Album
    • Video
  • Self Service
    • Member Portal
    • Billing Portal
    • QR-Codes
    • Portal Admin Form
  • Investments
    • Real Estate
    • Industial Investment
  • Tenders
    • General Procurement Notice
    • Awarded
    • Current Tender
  • e- Mrejesho
 
  Home   |   News Board
author image

PSSSF

To provide high quality social security services using competent, motivated staff and appropriate technology.

Benefit Types

  • Retirement Benefit
  • Death Benefit
  • Survivour Benefit
  • Maternity Benefit
  • Unemployment Benefit
  • Sickness Benefit
  • Invalidy Benefit

Online Services

  • Member Portal
  • Billing Portal
  • QR-Codes
Mha. Luhemeja amkaribisha Badru ofisi ya Waziri Mkuu
2024-02-19 00:00:00

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu; Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mha. Cyprian Luhemeja (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru, baada ya kumtambulisha kwa watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu. .

*Ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF

*Ahahidi ushirikiano, kulipa Pensheni kwa wakati,ukamilifu na usahihi

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu; Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mha. Cyprian Luhemeja amezitaka taasisi zote zilizo chini ya ofisi hiyo kuhakikisha zinatoa elimu juu ya kazi wanazofanya ili Wananchi waweze kuelewa majukumu yao vyema kwa la kupatiwa huduma.

Mha. Luhemeja amesema hayo Februari 20, 2024 katika kikao maalum cha kumtambulisha na kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma(PSSSF), Bw. Abdul-Razaq Badru kufuatia kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuingoza PSSSF.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru(kushoto) akiwa pamoja na Bw.John Mduma Mkurugenzi Mkuu wa WCF na Bi. Khadija Mwenda, Mtendaji Mkuu wa OSHA wakifatilia hotuba iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu; Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mha. Cyprian Luhemeja, wakati akimtambulisha Bw. Badru.

“Elimu juu ya taasisi zetu zote itolewe, haswa elimu ya Hifadhi ya Jamii iende kwa nguvu kwa wadau, naamini elimu ya Hifadhi ya Jamii ikieleweka vyema watu wengi hawatapoteza muda kwenye uwekezaji usio na tija” alisema Mha. Luhemeja.

Akimkaribisha Bw. Badru, Mha. Luhemeja alisema, “Ndugu zangu naomba muungane nami kumkaribisha Bw. Badru ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuongoza PSSSF, naomba tumpatie ushirikiano ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake, Bw. Badru hii ndio timu yako sasa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, karibuni sana”.

Mha. Lumemeja alifurahiswa na kauli ya Bw. Badru kuwa mwelekeo wa utendaji lazima uendane na kusudio na lengo la uwepo wa taasisi husika.

“Kweli nimefurahishwa na hoja ya Bw. Badru, kwamba ili utendaji kazi uende vyema ni lazima mwelekeo ulenge kusudio na lengo la taasisi husika, hivyo kila mmoja wetu ni lazima ajue mwelekeo wa taasisi yake ili aweze kufikia malengo” alifafanua Mha. Luhemeja.

Kwa upande wake, Bw. Badru alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF,ameahidi utendaji bora kwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru akizungumza baada ya kutambulishwa kwa kwa watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

“Kwa kweli nashukuru kwa kuwa sehemu ya timu hii chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, ninahidi ushirikiano kwenu ili kwa pamoja tuweze kutekeleza vyema majumu yetu” alisema Bw. Badru.

Bw. Badru alisema, PSSSF imejipanga kutekeleza vyema majukumu yake na kuendelea kutoa huduma bora kwa Wanachama kwa kuendelea kutumia TEHAMA ili kila mwanachama afikiwe kwa wakati.

“Tutaendelea kutoa elimu mahususi kwa Wanachama ili waelewe zaidi juu ya PSSSF, tunahakikisha kila mdau atafikiwa na tunaahidi kulipa pensheni kwa wakati, ukamilifu na usahihi” aliahidi Bw. Badru.

Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Februari 6, 2024 alimteua Bw. Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF.

About PSSSF

The main purpose is to collect contributions and payment of terminal benefits to employees of public service.The act shall apply in mainland Tanzania.


READ MORE

Quick Links

  • Billing Portal
  • Member Portal
  • Employer Portal
  • Announced Tenders

Get In touch

  • PSSSF House HQ , Makole, Dodoma
  • P.O.BOX 1501
  • info@psssf.go.tz
  • 0800 110040
  • Mon - Fri 8.00 - 17.00. Sat,Sun CLOSED

Zonal Offices

  • Dodoma: +255 26 2323338
  • Ilala: +255 22 2120912
  • Kinondoni: +255 22 2123848
  • Temeke: +255 22 2861039
  • Mwanza: +255 28 2506114
  • Mbeya: +255 25 2502243
  • Arusha: +255 27 2970284
  • Morogoro: +255 23 2934188
  • Mtwara: +255 23 2334661
  • Geita: +255 28 2520470
Copyright © 2024 psssf. All rights reserved.
  • Contact Us
  • Privacy Policy
  • Services
  • Disclaimer