PSSSF yatoa elimu ya UKIMWI, magonjwa yasiyoambukizwa kwa Watumishi wake
Na Mwandishi Wetu, Singida Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umefanya mafunzo kuhusu Ukimwi na Magonjwa yasiyoambukiza, mafunzo hayo yamefanyika katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kilichopo mkoani Singida kuanzia Aprili 20 hadi 22. Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bi. Esther Mwamyalla alimshukuru Mkurugenzi Mkuu pamoja na Menejimenti kwa kuratibu mafunzo hayo ili kuwawezesha Watumishi kupata uelewa juu ya UKIMWI na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo mara nyingi huwapata watumishi [...]

Na Mwandishi Wetu, Singida
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umefanya mafunzo kuhusu Ukimwi na Magonjwa yasiyoambukiza, mafunzo hayo yamefanyika katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kilichopo mkoani Singida kuanzia Aprili 20 hadi 22.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bi. Esther Mwamyalla alimshukuru Mkurugenzi Mkuu pamoja na Menejimenti kwa kuratibu mafunzo hayo ili kuwawezesha Watumishi kupata uelewa juu ya UKIMWI na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo mara nyingi huwapata watumishi walipo makazini pamoja na jamii zinazowazungunguka.
Magonjwa hayo yasiyoambukizwa ni pamoja na Kisukari, Shinikizo la Damu, Kiharusi, Kansa, Pumu, Figo na mengineyo ambayo huweza kumpata mtu yoyote pasipo kuambukizwa kutoka kwa binadamu mwenzake. Magonjwa yasiyoambukizwa hupatikana aidha kwa mabadiliko ya mwili kutokana na umri, jinsia, kazi na mazingira au kwa mtu husika kutofuata taratibu mbalimbali za afya bora.

