NA MWANDISHI WETU, SABASABA
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumisi wa Umma (PSSSF) CPA. Hosea Kashimba amesema zaidi ya wanachama wapatao 826 wamehudumiwa na PSSSF kwenye maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam tangu yalipoanza Julai 1 hadi leo Julai 10, 2020.

Bw. Kashimba ameyasema hayo leo Julai 10, 2020 wakati alipotembelea viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam ambako ndiko kunakofanyika maonesho hayo yaliyopewa kauli mbiu isemayo “Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu.

“Tuko katika banda namba 13 tuliloliandaa kwa ushirikiano na NSSF kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wanachama wetu, tunatarajia tutaendelea kuwahudumia wanachama zaidi hadi hapo maonesho yatakapofikia kilele chake, tunawakaribisha wanachama wetu na wananchi kwa ujumla. Hapa sabasaba tuna ofisi kamili .” Alisema Bw. Kashimba.

Alisema huduma zote zinazotolewa kwenye ofisi za PSSSF zilizoeneo nchi nzima zinapatikana kwenye banda hilo na kuwahimiza wanachama na wananchi kufika ili wahudumiwe.

“Mwanachama atapata huduma zote kama anataka kupata ufafanuzi kuhusiana na uanachama wake, kuhakiki taarifa zake, kuangalia yake na mambo yote yanayohusiana na uanachama huduma zinapatikana hapa.” Alisisitiza.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, CPA. Hosea Kashimba akimhudumia Bi. Immaculate Kagoro, mwanachama aliyetembelea banda la PSSSF Julai 10, 2020 katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, CPA. Hosea Kashimba akifafanua jambo kwa  Bi. Immaculate Kagoro, mwanachama aliyetembelea banda la PSSSF Julai 10, 2020 katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea