*DG: Tuendelee kutoa huduma bora

*Tutumie teknojia na mtandao wa ofisi kutoa huduma bora

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Wakati wiki ya huduma kwa Wateja inaanza leo, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA. Hosea Kashimba, amewataka Watumishi wa Mfuko kuendelea kutoa huduma bora kwa Wanachama na Watanzania kwa jumla.

Mkurugenzi Mkuu amesema hayo katika salaam zake kwa Watumishi wa Mfuko ikiwa ni ishara ya kuzindua wiki ya Huduma kwa Wateja kwa PSSSF. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Nguvu ya Huduma.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba akimhudumia mmoja wa wanachama aliyefika katika ofisi za PSSSF makao makuu, jijini Dodoma.

“Naomba tuwe na upendo, tujiamini na kujali. Popote ulipo unaweza kumsikiliza na kumhudumia vyema Mteja,” alisisiza CPA. Kashimba.

CPA. Kashimba amewashauri Watumishi watumie teknolojia na mtandao wa ofisi katika kuhakikisha Wanachama wanapata huduma bora popote walipo. Mkurugenzi Mkuu aliongeza, “Tuhakikishe mteja akitoka katika ofisi awe amehudumiwa vyema.

Wiki ya Huduma kwa Wateja inaadhimishwa ulimwengu kote kuanzia Oktoba 4 hadi 8 ya kila mwaka, lengo likiwa ni kuwakumbusha wajibu wao watoa huduma.