Na Mwandishi wetu Dar es Salaam,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amefanya ziara katika Mradi wa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (Accountacy Professional Center-APC) uliopo Bunju, mkoani Dar es Salaam, unaomilikiwa kwa ubia kati ya NBAA na PSSSF siku ya Jumamosi tarehe 19 Juni 2021.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akioneshwa baadhi ya maeneo ya mradi alipotembelea, aliyenyoosha mkono ni Mkurugenzi Mtendaji wa APC Bw. Wenceslaus Mkenganyi.

Katika ziara hiyo Waziri Mhagama alipata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali za mradi huo ikiwemo Hoteli, kumbi za mikutano, bwawa la kuogelea na uwanja wa mpira wa kikapu, ambapo alivutiwa na uwekezaji huo mkubwa. “Kuwepo kwa kituo hiki cha APC kimeweza kutoa Ajira na kusisimua Uchumi wa Nchi”, alisema Mhagama.
Waziri  Mhagama alifanya kikao na uongozi wa APC, PSSSF na NSSF. Katika kikao hicho Waziri Mhagama alitoa maelekezo mbalimbali kuhusu uendelevu wa kituo hicho kwa uongozi wa APC, PSSSF na NSSF  ambapo uongozi huo uliahidi kuyatekeleza.
MATUKIO KATIKA PICHA:

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikakagua moja ya Vyumba vilivyopo APC.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikagua moja ya vyumba vilivyopo APC.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikagua moja ya kumbi za mikutano zulizopo APC, kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Fortunatus Magambo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiongea na mmoja wa wapishi wa Hoteli ya APC.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikagua moja ya kumbi za mikutano zilizopo APC.

Moja ya kumbi za mikutano zilizopo APC.

Bwana la Kuogelea lililopo APC.

Uwanja wa pikapu uliopo APC.