Na Mwandishi Wetu Same

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amewapongeza wakulima wa zao la tangawizi na kukemea kilimo cha mirungi Wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro.

Ametoa pongezi hizo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata tangawizi cha Mamba Miamba kilichopo katika Kata ya Myamba Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Januari 7, 2021.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wananchi wa Kata ya Myamba Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro alipotembelea na kukagua ujenzi wa kiwanda cha kuchakata Tangawizi cha Mamba Miamba tarehe 7 Januari, 2021.

Waziri Mhagama alifurahishwa na wakulima hao kuwekeza katika kilimo cha tangawizi na kueleza kuwa, ni wakati muafaka kuachana na kilimo cha mirungi kwani Wilaya hiyo imekuwa ikijihusisha na kilimo hicho kwa muda mrefu. “Wakulima shikamaneni na hakikisheni kilimo cha tangawizi kina kuwa na tija na kuachana kabisa na kile cha mirungi, maeneo yenu yana rutuba ya kutosha kwa kilimo yatumieni kuzalisha kwa wingi tangawizi mjikwamue kiuchumi,” alisema Waziri Mhagama.

Aliongezea kuwa, katika maeneo yaliyokuwa yakimpa shida kwenye mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi ni pamoja na wilaya hiyo. “Faraja ninayoipata leo ni kuona zao la tangawizi sasa linakwenda kuchukua nafasi ya kilimo cha mirungi na niwaombe Kamati ya Ulinzi na Usalama tujitahidi kuhakikisha tunatokomeza ulimaji wa mirungi kwa gharama yoyote” alisisitiza.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Anne Malechela alieleza furaha yake kwa ujio wa Waziri kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho huku akiahidi kuendelea kushirikiana na uongozi wa Mkoa na wananchi kuhakikisha kiwanda kinakuwa na maendeleo endelevu ili kuleta matokeo chanya kwa wakazi wa Same na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA Hosea Kashimba alieleza namna walivyodhamiria kuwekeza katika kiwanda hicho na kuhakikisha kinaendelea kwa miaka mingi na kuleta tija. “Katika Kiwanda hiki tumewekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 1.8 kwa kuweka mtaji, na kufanya ukarabati wa majengo, kujenga uzio unaozunguka kiwanda pamoja na mifumo ya umeme  kurahisisha shughuli za uendeshaji wake,” alieleza CPA Kashimba

Aliongezea kuwa  hadi Desemba 2020 Mfuko umetoa shilingi bilioni 1.3 za Kitanzania zilizotumika kununua mitambo ya kisasa, kufunga mifumo ya umeme kutoka TANESCO, Ukarabati wa jengo na kufunga mashine ambapo hatua hiyo imefikia asilimia 85.

Sambamba na hilo alieleza kuwa  Kiwanda kitasindika tangawizi hadi tani 10 kwa siku na kusambaza bidhaa zake katika soko la ndani na nje ya nchi ambapo kitauza unga wa tangawizi katika nchi za Kenya, Uganda , Malawi, Afika Kusini, Uholanzi na nchi za Bara la Asia.

Mkurugenzi alibainisha ajira rasmi kati ya 30 na 40  zinatarajiwa kuzalishwa pindi uzalishaji wa Kiwanda utakapoanza, ambapo itaongeza tija kwa vijana na kutoa wito kuichangamkia fursa ya uwepo wa kiwanda hicho.

MATUKIO KATIKA PICHA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mbunge wa Same Mashariki.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa umma (PSSSF) Bw. Hosea Kashimba akieleza namna mfuko ulivyowekeza katika kiwanda cha kuchakata tangawizi cha Mamba Miamba kilichopo Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo ya michoro ya ramani ya kiwanda cha kuchata Tangawizi cha Mamba Miamba kutoka kwa Mhandisi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Simon Marandu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye ziara kiwanda ya kikazi katika kiwanda cha Kuchakata tangawizi cha Mamba Miamba, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Same

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo ya kıwanda kutoka kwa Mhandisi wa PSSSF Bw. Iddi Mvungi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mtambo ulionunuliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ( PSSSF) kwa ajili ya kuchakata tangawizi katika kiwanda cha Mamba Miamba kilichopo wilaya ya Same.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) akihutubia wananchi wa Kata ya Myamba Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro alipotembelea na kukagua ujenzi wa kiwanda cha kuchakata Tangawizi cha Mamba Miamba tarehe 7 Januari, 2021.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) akihutubia wananchi wa Kata ya Myamba Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro alipotembelea na kukagua ujenzi wa kiwanda cha kuchakata Tangawizi cha Mamba Miamba tarehe 7 Januari, 2021.

Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Fortunatus Magambo (aliyekaa katikati) akifuatilia maelezo yaliyokuwa yakisomwa na Bw. Mbaraka Ally (hayupo pichani). Kushoto ni Meneja Miradi ya Majengo Bw. Marco Kapinga.