Na: Mwandishi wetu – Kilimanjaro

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, amepongeza uwekezaji kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na Jeshi la Magereza Tanzania kwa hatua nzuri ya ukamilishaji wa kiwanda cha uzalishaji bidhaa za Ngozi cha Waziri Kilimanjaro (Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd).

Waziri Ndalichako ametoa pongezi hizo hivi karibuni baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kukagua maendeleo ya kiwanda na kuangalia namna ya uzalishaji wa bidhaa. Alisema kuwa, amefurahishwa na uwekezaji katika kiwanda hicho ambacho kitatoa ajira nyingi kwa vijana pamoja na kuchangia ukuaji wa pato la Taifa kupitia bidhaa zitakazo kuwa zinazalishwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro, Mhandisi. Masud Omari ameeleza kuwa Menejimenti ya kiwanda imejipanga kuendelea kukuza masoko ya bidhaa zinazozalishwa ili kuhamasisha soko la ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia), akiangalia kiatu cha ngozi alipotembelea Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Prof. Jamal Katundu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro, Mhandisi. Masud Omari Sambamba na hayo ameupongeza Uongozi wa Chuo cha VETA pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) kwa kutoa mafunzo bora kwa vijana ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi, huku akibainisha kuwa vijana wanaotoka katika vyuo hivyo wamekuwa watengenezaji wazuri wa viatu. Hivyo, alitoa wito kwa vijana kuchangamkia sekta ya ngozi kwa kuwa Serikali imeanza uwekezaji na kutakuwa na uhitaji wa rasilimali watu.

Mhandisi Msimamizi wa Mradi Eng. Sp. Emmanuel Mwangalaba akielekeza jambo kuhusiana na maendeleo ya mradi katika ziara iliofanywa na Mhe. Ndalichako katika Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, akifanya mazungumzo na Uongozi wa Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro hivi karibuni.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu), Prof. Jamal Katundu, akichangia jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alipotembelea Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro, Mhandisi. Masud Omari, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.