*Ni ya kuwajengea uwezo katika manunuzi

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Watumishi wa Mfuko wa PSSSF wanahudhuria mafunzo ya siku tano, kuanzia Aprili 12 hadi 16, 2021 katika ukumbi wa NSSF mkoani Morogoro.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mfuko, yanaendeshwa na Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi. Yamejikita kutoa elimu katika mchakato yakinifu wa uchambuzi na majadiliano kwa kuzingatia Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011, Kanuni zake za mwaka 2013 kama zilivyoboreshwa mwaka 2016, 2018 na 2017.

Watumishi wa PSSSF wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa mafunzo hayo Bw. Azizi Kilongole (wa nne kutoka
kulia) pamoja na Amos K. Mang’ombe (wa nne kutoka kushoto).

Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi katika eneo la ununuzi katika Mfuko.

Mafunzo hayo yanahudhuriwa na wawakilishi kutoka Kurugenzi zote za mfuko, yaani Kurugenzi ya Uendeshaji, Uwekezaji, Fedha, Tehama, Utawala na rasilimali watu na Ununuzi na Ugavi.

Pia yamehusisha Wakaguzi wa ndani na Wanasheria ambao ni wasimamizi na washauri wa Mfuko katika utekelezaji wa majukumu ya Mfuko kwa kuzingatia sheria na kanuni mbalimbali.

Mkufunzi kutoka Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi Bw. Azizi Kilonge akifundisha Watumishi wa PSSSF katika semina inayofanyika kwenye Ukumbi wa NSSF mkoani Morogoro.

Watumishi wa Mfuko wa PSSSF wakifuatilia semina hiyo inayofanyika katika ukumbi wa NSSF mkoani Morogoro.

Watumishi wa Mfuko wa PSSSF wakifuatilia semina hiyo inayofanyika katika ukumbi wa NSSF mkoani Morogoro.

Watumishi wa Mfuko wa PSSSF wakifuatilia semina hiyo inayofanyika katika ukumbi wa NSSF mkoani Morogoro (Picha zote na PSSSF).