Moro: Mfuko ufanye uwekezaji wenye tija

Pwani: Tunatoa huduma bora kila siku

Na Waandishi Wetu, Morogoro na Pwani

Wanachama wa Mfuko katika mikoa ya Morogoro na Pwani wanazidi kufurahia huduma mbalimbali za Mfuko ambazo anazipata karibu na bila tatizo lolote.

Hayo yalisemwa kwa nyakati tofauti na Bw.Lulyalya Sayi Meneja wa Mfuko mkoa wa Morogoro na Bibi. Maria Lupondo Meneja wa mkoa wa Pwani katika mahojiano maalum na waandishi wa Habari Mafao hivi karibuni katika mikoa yao.

“kwa kweli wanachama wanafurahia kusogezwa kwa huduma karibu yao, na pia wanafurahia kulipwa kwa wakati kwa mafao yanayolipwa mkoani,” alisema Bw. Sayi.

Meneja Mkoa wa Morogoro Bw Sayi Lulyalya akiwa na watumishi wa Mfuko akiwalekeza jambo.

Kwa upande wake Meneja wa Mfuko mkoani Pwani, Bibi Lupondo alisema, “Wanachama wa iliyokuwa PPF, GEPF na LAPF wanafurahia huduma kwani zamani kuliwa na ofisi za PSPF tu, hivyo baada ya mifuko kuunganishwa sasa wote wanapata huduma katika ofisi yetu”.

Meneja wa Mfuko Mkoa wa Pwani, Bi. Maria Lupondo

Kwa upande wa mkoa wa Morogoro, Bw. Sayi alisema wengi ya wanachama wanaokwenda kupata huduma za; mafao ya uzeeni, mirathi, pensheni ya mwezi, fao la uzazi, fao la kukosa ajira na fao la elimu.

“Wanachama wetu mkoani kwetu wanashauri uwekezaji wa Mfuko ufanyike kwa umakini na tuwekeze maeneo salama na yenye tija kwa Mfuko” alisema Bw. Sayi.

Kwa upande wa mkoa wa Pwani, Meneja wa mkoa huo Bibi. Lupondo alisema, “wanachama wengi wanakuja kupata huduma mbalimbali hususani kupata taarifa za michango na kufatilia taarifa za mafao mbalimbali”.

Hata hivyo Bibi Lupondo alisema wanachama wa mkoa wa Pwani wanashauri fomu mbalimbali za Mfuko ziadikwe pia kwa lugha ya Kiswahili ili iwe rahisi kuzielewa na kujibu vyema.

“Tunashukuru sana, kwani ofisi yetu tuna mahusiano mazuri na watendaji mbalimbali wa mkoa akiwemo Mkuu wa mkoa mwenyewe…Pwani tunajivunia huduma nzuri kwa wanachama, wetu hatuna wiki ya utumishi wala wiki ya huduma kwa wateja, kwetu sisi wanachama kila siku wanapata huduma bora,” aliweka wazi Bibi. Lupondo.