Na Mwandishi Wetu MOSHI

Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama ameagiza wabia wa Kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro kuhakikisha wamekamilisha   jengo la kuchakata ngozi  kwa wakati.

Akizungunza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho, Waziri  Mhe. Jenista Mhagama alisema Serikali imeshajipanga kuhakikisha  inaboresha uzalishaji wa bidhaa za ngozi hivyo kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia  ukuaji wa soko la uhakika miongoni mwa wadau wa ngozi. Mhe. Mhagama alisema anataka kiwanda kuwa endelevu ili Tanzania iweze kujivunia kuwa na kiwanda kikubwa ambacho kitaweza kuongoza Afrika Mashariki na Kati.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo kwa watendaji wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro wakati wa ziara yake kiwandani hapo.

“Mapema Septemba  2020, Serikali ilikutanisha  wadau wazalishaji wa ngozi, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo pamoja na   Wizara yangu katika kongamano lililofanyika Jijini Mwanza kwa lengo la kujadili na  kuangalia namna  ya kumaliza matatizo yanayopelekea kukwamishwa kwa uzalishaji wa ngozi bora, “alisema Mhe. Mhagama

Kwa upande wa masoko Mhe. Mhagama amepongeza Uongozi wa Kiwanda kwa hatua ambayo wamefikia ya kupata oda ya viatu pea 48,000 za viatu. “Kwa hiyo ni lazima tuwe na kiwanda cha kuchakata ngozi ambapo tutakuwa na uhakika wa kuwa na ngozi zenye ubora unaotakiwa kuzalisha viatu bora”,  alisisitiza Waziri Mhagama

Pia alifurahishwa na suala la ajira ambapo mchakato wa ajira 1600 unaendelea. “Ikiwa tutaenda sawa na ratiba ya ukamilikaji wa kiwanda, ifikapo mwezi Juni, 2021, tutapata waajiriwa wapya” alifafanua Mhe. Mhagama

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipokelewa na Watendaji wa usimamizi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba   alisema  wamechukua maelekezo ya Mhe. Waziri ya kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati, “kama wabia wa mradi tutahakikisha mkandarasi hapungukiwi na malighafi”. CPA Kashimba alisema mradi ukikamilika utaweza kutoa ajira zaidi ya 3000 na uzalishaji uweze kuchochea uchumi wa Nchi  na kupata faida ambayo itaweza kurudisha fedha za wanachama ambazo zimewekezwa kwenye kiwanda hiki. Pia alimshukuru Mhe. Waziri kwa jinsi alivyoweza kujitoa kwa kupita na kuona na kuweza kutoa maelekezo ili kuhakikisha mradi huu unakamilika vizuri.

Kwa upande wake  Mkuu wa Magereza Mkoa wa Killimanjaro, Miraji Katumbily, alisema tayari wamepokea agizo hilo na watalifanyia kazi kwa muda uliopo.

Kwa upande wake,  Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro,  Mhandisi Masaud Omary, alisema  ujenzi wa jengo la kuchakata ngozi umekamilika kwa asilimia 40  na kuhaidi watalikamilisha kwa wakati . “Jengo  la kuchakata ngozi litakuwa limekamilika katika kipindi cha Januari mpaka Juni, 2021, na tumeshatoa ajira 250 na hadi kufikia mwezi Juni tutakuwa tumetoa ajira  zaidi ya 1600,” alisema Mhandisi Omary.

Kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro kinachomilikiwa kati ya  ubia wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Jeshi la Magereza, kilifunguliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   kinatarajia kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 3,000 mara baada ya kukamilika.

MATUKIO KATIKA PICHA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika ziara hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia hatua za ujenzi wa kiwanda cha kuchakata bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro alipotembelea kujionea maendeleo ya mradi huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye ziara na timu aliyoongozana nayo katika kiwanda cha viatu cha Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo kwa watendaji wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro wakati wa ziara yake kiwandani hapo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye ziara na timu aliyoongozana nayo katika kiwanda cha viatu cha Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye ziara na timu aliyoongozana nayo katika kiwanda cha viatu cha Kilimanjaro.

Moja ya Jengo la Kuchakata Ngozi linaloendelea kujengwa.

Moja ya jengo linaloendelea kujengwa katika kiwanda hicho cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro.