Na mwandishi wetu, Mwanza

Usimamizi wa bora wa mikataba utaepeusha migogoro katika mchakato wa ununuzi na kusaidia Mfuko kupata thamani ya fedha katika ununuzi.

Haya yamebainika katika mafunzo ya awamu ya pili ya Usimamizi wa Mikataba na Miradi yaliyotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) jijini Mwanza.

Akizungumzia mafunzo hayo, Meneja wa Ununuzi na Ugavi, Bi. Amina Kipingu, alisema mafunzo haya yatawasaidia kuondoa migogoro mbalimbali ya kimikataba. “Ili kuweza kuwa na mikataba bora katika Taasisi yetu, kila mhusika anapaswa kujua nini wajibu wake, wakati wa uandaaji wa mikataba ili kuweza kufanikisha malengo ya Taasisi” alifafanua Bi. Kipingu. Vilevile Bi. Amina Kipingu, alishukuru kwa kupata mafunzo ambayo yatasaidia kuweza kuwa na uelewa wa pamoja.

Watumishi wa Mfuko waliohudhuria mafunzo ya usimamizi wa Miradi na Mikataba awamu ya pili, wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Utawala Bi. Esther Mwamyalla (aliyekaa katikati), Mwelelekezi – Usimamizi wa Mikataba na Miradi, Bw. Paul F. Basondole (aliyekaa kulia) na Dereck N. Mbanzendole (aliyekaa kushoto).

Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Meneja wa Kanda ya Ziwa Mashariki, Bw. Godfrey Mollel, ametoa pongezi kwa PSSSF na wote waliohudhuria mafunzo hayo muhimu kwa ufanisi wa Mfuko.

“Nina imani mmejifunza mengi katika usimamizi wa mikataba na miradi” alifafanua Bw. Mollel. Alisema “tukiheshimu mafunzo haya na kuyaishi, nina uhakika mambo yatakuwa mazuri kwenye taasisi na kwetu sisi wenyewe na tuheshimu uamuzi wa Menejimenti wa kuwaweka pamoja, kujifunza, pamoja na kujadiliana pamoja juu ya mafunzo haya ambayo ni muhimu sana”.

Kwa upande wa mkufunzi wa mafunzo, Bw. Dereck Mbanzendole, alisema wamewajengea uwezo wa kuandaa mikataba washiriki wa mafunzo hayo, ambayo utawasaidia kuwa na mikataba bora, kwa sababu mkataba ukiwa umeandaliwa vizuri hata usimamizi wake huwa mwepesi na rahisi.

Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uwezo watumishi wa PSSSF juu ya usimamizi wa mikataba ya wakandarasi (wahandishi washauri) ambapo Serikali itapata thamani ya fedha katika usimamizi wa miradi na kuepusha migogoro katika miradi.

Mwelelekezi – Usimamizi wa Mikataba na Miradi, Bw. Paul F. Basondole akifundisha katika mafunzo hayo.

Watumishi wa PSSSF wakijali jambo wakati wa semina hiyo.

Watumishi wa PSSSF wakifuatilia mafunzo hayo.

Mwelelekezi – Usimamizi wa Mikataba na Miradi, Dereck N. Mbanzendole akifundisha katika mafunzo hayo.

Meneja wa Kanda ya Ziwa Mashariki, Bw. Godfrey Mollel akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF.