*Mkurugenzi aongoza kuchanja

*Bonanza la Wafanyakazi lafana

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetumia tamasha la michezo ya Watumishi kwa ajili ya kutoa elimu ya UVIKO-19 kwa lengo la kuhamasisha Wafanyakazi wa kupata chanjo.

Elimu hiyo ya UVIKO 19 ilitolewa na Mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma Bw. Andrew Method, Oktoba 2, 2021 katika tamasha la watumishi wa Mfuko lililokutanisha watumishi kutoka ofisi ya Makao makuu na ofisi ya mkoa wa Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (wa kwanza kushoto) akifanya jogging pamoja na watumishi wa PSSSF wakati wa bonaza lililofanyika siku ya jumamosi tarehe 02 Oktoba 2021, jijini Dodoma katika chuo cha CBE Dodoma.

Akizunguzia umuhimu wa elimu hiyo ya UVIKO-19, Meneja Utawala Bibi. Esther Mwamnyalla Mfuko alisema, “Lengo ni kuboresha afya zetu na leo katika kuchanja tutaongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala Bw.Paul Kijazi. Kwa hiyo vijana wote mjitokeze, chanjo hii si kwa Wazee na vijana vilevile, vijana ni taifa la kesho usingojee kufa leo, kufa kesho”

Kwa upande wake mtoa elimu ya UVIKO-19 Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt. Andrew Method, alisema ukipata chanjo inazuwia kwa asilimia kubwa kutopata maambukizi na ikitokea mtu akipata maambukiza hatohitaji masaada wa oxygen.

Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala Bw. Paul Kijazi akipatiwa chanjo wakati wa bonaza lililofanyika siku ya jumamosi tarehe 02 Oktoba 2021, jijiji Dodoma katika chuo cha CBE Dodoma.

“Kwa hiyo niombe tutumie hii nafasi, kwasababu ili tuweze kuwa huru ni lazima tuchanje zaidi ya asilimia sitini ya population. Kwahiyo ni muhimu tujitokeze, tuwashauri na wengine wajitokeze ili waweze kupata chanjo” alililisitiza Mganga Mkuu.

Kwa upande wake, Mkuu wa PSSSF CPA. Hosea Kashimba, akizungumzia tamasha la mchezo la Wafanyakazi alisema, “Bonaza hili ni sehemu ya kumuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba tunakuwa na taifa lenye watu wenye afya njema, PSSSF ni sehemu ya watoa huduma, hivyo maratajio yetu tukiwa na njema tutatoa huduma bora zaidi”.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (wa kwanza kushoto) akitoa kombe kwa washindi wa jumla wa michezo yote katika bonanza hilo lililofanyika katika chuo cha CBE Dodoma, Oktoba 02, 2021.

Katika tamasha hilo washindi wa jumba walikuwa Siafu (mshindi wa kwanza), Faru (mshindi wa pili), Mbuni (mshindi wa tatu) na nyuki (mshindi wa nne). Michezo ilijumuisha michezo ifuatayo; mazoezi ya viungo, mbio fupi, mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa pete, kuvuta kamba, karata, draft na kumkimbia kwenye magunia.

“Bonanza lilikuwa zuri sana, tulijichanganja na watu tuliokuwa hatuafahamiani kwa karibu na tulifurahi pamoja” alisema Bw. Edward Temu wa Kurugenzi ya Fedha.

Mkurugenzi Mkuu CPA. Hosea Kashimba akikagua moja ya timu ya mpira wa miguu katika bonanza hilo lililofanyika katika chuo cha CBE Dodoma,Oktoba 02, 2021.

Baadhi ya watumishi wa PSSSF Makao Makuu pamoja na Mkoa wakicheza draft katika bonanza lilifonyika katika chuo cha CBE Dodoma,Oktoba 02, 2021.