Na Mwandishi Wetu, Simiyu

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umejumuika na Wanawake wote ulimwenguni katika kuadhimisha siku ya Wanawake ambayo kitaifa ilifanyika mkoniani Simiyu na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

PSSSF iliwakilishwa na watumishi Wanawake, wakiongozwa na Meneja Kiongozi (Uhusiano na Elimu kwa wanachama) Bibi. Eunice Chiume, pamoja na Meneja Utawala Bibi Esther Mwamyalla.

“Kwa kweli tumefurahi kuungana na wanawake wengine ulimwenguni katika kuadhimisha siku hii muhimu kwetu” alisema Bibi. Mwamyalla.

Kwa upande wake, Meneja Kiongozi, Bibi Chiume aliwakumbusha watumishi wanawake wa PSSSF kufanyakazi kwa ufanisi na kwa kushirikiana kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wanachama wa Mfuko.

“Pamoja na kufanyakazi za Mwajiri, nawaomba wanawake wote kuhakikisha tunaendeleza jukumu letu la msingi la kutunza familia zetu, kwa kufanya hivyo tutakuwa tunajenga taifa bora la Tanzania” alishauri Bibi. Chiume.

 

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hufanyika Machi 8 kila mwaka. Kauli mbiu yam waka huu ilikuwa Kizazi cha Usawa Kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na Baadae.