*Ni katika maonesho ya madini

Na Mwandishi Wetu, Geita

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepata tuzo ya mtoa huduma bora katika sekta ya Hifadhi ya jamii katika Maoenesho ya nne ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika mkoani Geita hivi karibuni.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alitoa pongezi kwa ushindi huo na kuongeza, “Katika maonesho yeyote tunayoshiriki tulenge kufanya vizuri zaidi na kushinda. Hii inatupa nguvu”.

Watumishi wa PSSSF Mkoa wa Geita, wakiongozwa na Meneja wa ofisi ya Mkoa huo, Bw. Geofrey Kolongo kupokea tuzo kutoka kwa Mhe. Mwiguli Nchemba, Waziri wa Fedha aliyemwakilisha Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, katika ufungaji wa maonesho hayo.

Katika maonesho hayo Watumishi waliowakilisha Mfuko waliogozwa na Geoffrey Korongo ambaye ni Meneja wa mkoa wa Geita. Wengine ni Rehema Mkamba, Mariam Hincha, Violet Michael, Davidi Ngamesha, Robert Giloriti na Andrew Kwaleka

Maonesho hayo ya nne yalifunguliwa Septemba 22, 2021 na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa na kusema serikali imedhamiria kuhakikisha rasilimali za nchi zinachangia katika kuinua uchumi wa Watanzania. Yalifungwa Septemba 26, 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ambaye alimwakilisha Mheshimiwa Makamu wa Rais.

Baadhi ya Wananchi wakipata elimu katika banda la Mfuko wa PSSSF.

Katika hatua nyingine, Mfuko ulishiriki maonesho ya Bodi ya Wakaguzi wa Ndani (IIAT) yaliyofanyika Jijini Arusha kuanzia Septemba 20 hadi 24, 2021. Katika maonesho hayo Mfuko ulipatiwa cheti cha ushiriki.

Tuzo ya PSSSF iliyotolewa katika maonesho ya Bodi ya Wakaguzi wa Ndani.