*Ni kwa zaidi ya Watumishi 300

*Wapatiwa elimu mujarabu ya Mfuko

Na Mwandishi Wetu, Tanga

Maafisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wakiongozwa na Kaimu Meneja wa PSSSF mkoa wa Tanga Bw. Nyemo Chomola wametoa semina kwa Watumishi wa Mamlaka ya Bandari mkoa wa Tanga.

Kaimu Meneja wa Tanga, Bw. Nyemo Chomola akitoa mada kwa Watumishi wa Bandari Tanga, Katika semina iliyoandaliwa na Mfuko vivi Karibuni.

“Tunatoa shukrani kwa wenzetu wa Mamlaka ya Bandari, Tanga kwa kutupatia fursa ya kutoa elimu kwa Watumishi wa Mamlaka hiyo wasiopungua 300, mafunzo hayo yalifanyika Ijumaa Juni 4, 2021” alifafanua Bw. Nyemo.

Katika semina hiyo Bw, Nyemo aliambatana na watumishi wengine wa Mfuko ambao ni Bw. Hamidu Nassoro, Bw. Ponela Msola na Bibi. Irene Kahangwa, wote ni watumishi wa PSSSF ofisi ya mkoa wa Tanga.

Katika semina hiyo, Watumishi wa Bandari walieleweshwa juu ya PSSSF ikiwemo ufuatiliaji wamichango, mafao yanatolewa na sifa zake. Pia waliuliza maswali na kupatiwa ufafanuzi, jambo ambalo limesaidia kuongeza uelewa wao kuhusu haki na wajibu wao.

Mmoja wa Watumishi wa Bandari Tanga (wa pili kulia) akiuliza swali katika semina iliyofanyika hivi karibuni.

Bibi Irene Kahangwa, Afisa Matekelezo Ofisi ya PSSSF Tanga akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.

Maafisa wa PSSSF Tanga, wakiwa Katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Bandari Tanga, Katika semina iliyoandaliwa na PSSSF hivi karibuni.