Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Watumishi Wanawake wa kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wameungana na Wanawake duniani katika kuadhimisha siku ya kimataifa wa wanawake.

Watumishi wa kitengo cha Huduma kwa wateja PSSSF Makao Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na mwanachama, Hawa Hamisi Ramadhan aliyefika kupata huduma siku ya wanawake duniani.

Katika kuadhimisha siku hii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Doroth Gwajima (Mb) alitoa salaam pamoja na mambo mengine alisema “Nawahakikishia kuwa serikali ya Tanzania inajali wanawake na ipo mstari wa mbele kutekeleza mipango endelevu yenye nguzo za kisheria na kisera”

Baadhi ya mambo yaliyobainishwa na Mhe. Waziri ni pamoja na; kuwawezesha Wanawake kiuchumi kupitia mikopo ambapo alisema mwaka 2019/2020 imetoa mikopo ya thamani ya bilioni 23.8 kwa vikundi 6859, Serikali inatekeleza mpango wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake, Serikali haijawaacha nyuma wanawake kwenye nafasi za uongozi ngazi zote kuanzia Mhe. Makamu wa rais Mama Samia Suluhu, Mhe. Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Waheshimiwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi katika Wizara na Taasisi mbalimbali. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Wanawake katika Uongozi, Chachu Kufikia Dunia Yenye Usawa.

Meneja wa Huduma kwa Wateja, Bi. Laila Maghimbi akiwa ofisini kwake tayari kuwahudumia wateja katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Mkurugezi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, akizungumzia siku ya wanawake alisema, “Leo ni siku ya wanawake Duniani. Tunawapongeza sana. Wanawake wamekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi katika Familia, Taasisi na Taifa wa ujumla. Tunawaombea waendelee kuchapa kazi”.

Watumishi wa kitengo cha Call centre wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa majukumu yao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Dodoma, 8/3/2021.