MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSSF) wanashiriki maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam katika banda namba 13 lililopewa jina banda la ushirikiano kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Ushirikiano huo wa kutoa huduma pamoja umewarahisishia wanachama na wananchi kwa ujumla wanaofika kwenye maonesho hayo kwa lengo la kupata huduma itolewayo na mifuko hiyo.PSSSF ni muunganiko wa mifuko minne ya GEPF, LAPF, PPF na PSPF hivyo kumekuwa na kuhamishwa kwa wanachama kutoka mfuko mmoja kwenda mwingine kulingana na mabadiliko ya ajira ya muhusika.
Ikiwa muhusika amehama kutoka ajira ya sekta binafsi kwenda ya umma, basi atalazimika kwenda “meza” ya PSSSF na kama amehama kutoka ajiya ya utumishi wa umma kwenda sekta binafsi atalazimika kwenda “meza” ya NSSF, hayo ndiyo manufaa ya kutoa huduma kwenye banda moja.

Mapokezi ya banda la ushirikiano kati ya PSSSF pamoja na NSSF

Kaimu Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma PSSSF, Abdul Njaidi(wakwanza kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Kiongozi Mahusiano na Elimu kwa Umma (NSSF) Bi. Lulu Mengele

Bi.Elizabeth Shayo wa PSSSF (kulia) akimfafanulia jambo mwanachama aliyefika katika banda la PSSSF kupata huduma