Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma umeadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wake waliofika katika ofisi za PSSSF zilizopo katika mikoa 29 Tanzania.

 

PSSSF inatoa huduma kwa wateja katika ofisi zote za Mfuko nchini lakini pia wanachama wanaweza kupata huduma kwa kupiga simu bure, kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupitia mitandao ya kijamii.

 

“Ningependa kuwakumbusha watumishi wote wa Mfuko kuhusu umuhimu wa ushirikiano (team work) katika kuhakikisha wanachama wetu wanapatiwa huduma nzuri na ya kuridhisha. Watumishi tukumbuke kwamba huduma ya mteja wa nje haiwezi kufikia ubora iwapo huduma ya ndani haiko sawa. Kwa maneno haya, nawakumbusha watendaji wote tuwe kitu kimoja, tuheshimiane na tupeane ushirikiano katika kumkamilishia mahitaji ya yule anayekutana na mteja ili kufanikisha huduma bora kwa wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla”, alisisitiza Bw Hosea Kashimba, Mkurugenzi mkuu wa Mfuko.

Wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka huu imeadhimishwa kuanzia tarehe 7/10/2019 hadi tarehe 11/10/2019.