NA MWANDISHI WETU, MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ni miongoni mwa Taasisi za Umma zinazoshiriki kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyoanza leo Novemba 8, 2021 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa waandaaji wa maadhimisho hayo, Wizara ya Fedha na Mipango, walengwa wakuu ni pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo: watumishi wa umma; wanafunzi; wakufunzi; wanawake, vijana, watu wenye mahitaji maalumu; wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs); asasi za kiraia; Wahariri na waandishi wa vyombo vya habari; watoa huduma za fedha; na umma kwa ujumla.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa PSSSF Rehema Mkamba amesema, ushiriki wa Mfuko kwenye maadhimisho hayo unatoa fursa ya kukutana na wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla ambao watafaidika na kupata elimu kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mfuko.

“Majukumu ya msingi ya Mfuko ni pamoja na Kuandikisha Wanachama, Kukusanya Michango, Kulipa Mafao lakini pia Kuwekeza kwa njia ya hisa kwenye mabenki na kwenye maeneo mengine kwa mujibu wa sheria,” alifafanua Rehema na kuongeza…Kauli mbiu ya Wiki hii ni “Boresha Maisha kupitia elimu ya fedha.”  na kwa kuzingatia kaulimbiu hiyo, mwanachama au mwananchi akifika kwenye banda la PSSSF atapata elimu ya namna gani anaweza kufaidika na mikopo hiyo inayotolewa na PSSSF kwa kushirikiana na benki ya Azania.

Afisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Winfrida Jorry (katikati) akizungumza na wananchi waliofika kwenye banda la Mfuko huo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2021 ambako kunafanyika Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ili kupata elimu ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo ikiwemo fursa za kupata Mikopo ya nyumba na viwanja. Maonesho hayo yameandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango ili kuwawezesha wananchi kupata elimu kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya fedha. Kauli mbiu ya Wiki hiyo ni ” Boresha Maisha kupitia Elimu yab Fedha”

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF Rehema Mkamba (kushoto) na mwenzake, Coleta Mnyamani wakiwa tayari kuwahudumia wananchi.

Afisa Mafao Mwandamizi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Abdallah Juma (kulia)) akimkaribisha mwanachama wa PSSSF kwenye banda la Mfuko huo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2021 ambako kunafanyika Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ili kupata elimu ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo ikiwemo fursa za kupata Mikopo ya nyumba na viwanja. Maonesho hayo yameandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango ili kuwawezesha wananchi kupata elimu kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya fedha. Kauli mbiu ya Wiki hiyo ni ” Boresha Maisha kupitia Elimu ya Fedha”

Afisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Winfrida Jorry, akiwahudumia wanachama wa PSSSF.

Wanachama wa PSSSF wakipata huduma kwenye banda la Mfuko huo.

Afisa Mwandamizi wa Fedha, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Edward Temu (kulia) akifurahi kwa pamoja na Mwanachama wa Mfuko huo aliyefika kuhudumiwa kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Novemba 8, 2021.

Deogratius Marwa, Afisa Matelekezo Mwandamizi, PSSSF, akipitia taarifa za Mwanachama aliyetaka kujua kiwango alichochangiwa na mwajiri wake.