Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma unashiriki katika maonesho ya usalama na afya mahala pa Kazi yanayofanyika katika viwanja.vya kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Katika maonesho hayo taasisi mbalimbali zinaonesha jinsi zinavyozingatia usalama na afya mahala pa kazi kwa watumishi wake.

Mrisho Mpoto (wa pili kutoka kushoto) akiwa amevaa moja ya viatu vinavyozalishwa na Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro.

Baadhi ya wastaafu wa PSSSF wakipata taarifa mbalimbali zinazohusu Mfuko.

Katika banda la PSSSF pamoja na.huduma.nyingine mwanachama wa PSSSF anaweza kupata taarifa za michango, Pensheni na kufatilia madai.

Pia katika banda la PSSSF, kiwanda cha kimataifa cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro kinaonesha na kuuza bidhaa zake mbalimbali, ikiwemo viatu maalum kwa ajili ya wafanyakazi wa viwandani na migodini.

Maonesho haya yanaratibiwa na Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA)