NA MWANDISHI WETU, SIMIYU

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeanza rasmi kulipa Fao la Uzazi kwa wanachama wake wanawake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Angellah Kairuki ameelezwa hayo alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu Agosti 3, 2020.

Afisa Mkuu wa Mafao PSSSF, Bw. Daniel Dugilo amemueleza Mhe. Waziri kuwa PSSSF imeanza rasmi kulipa Mafao hayo ambayo yalisita kufuatia Serikali kuuunganisha mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, PPF, LAPF, na GEPF.

“Mhe. Waziri napenda pia niseme kuwa PSSSF imeanza rasmi kulipa fao la uzazi kwa wanachama wetu wanawake, itakumbukwa kwamba ulipaji wa fao hili ulisitishwa kwa muda kutokana na kuunganishwa kwa mifuko.” Alisema Dugilo.

Akifafanua zaidi kuhusu vigezo vinavyozingatiwa kulipa fao hilo, Kaimu Meneja wa PSSSF mkoa wa Mara, Bi.Nyaswi Elias alibainisha kuwa ni lazima mfaidika awe ni mwanachama wa PSSSF mwanamke aliyechangia kwa miezi 36 sawa na miaka mitatu (3) na anapaswa kuwasilisha nyaraka zote zinazohitajika kwenye mfuko ndani ya siku Tisini (90) baada ya kujifungua.

Masharti hayo alisema, “Fao hilo la uzazi mwanachama anaweza kufaidika nalo kwa uzao wa kwanza, wapili, watatu hadi wanne haijalishi katika moja ya uzao huo kajifungua mtoto mmoja au mapacha au kila uzao kajifungua mapacha, tunachozingatia hapa ni kwamba mwachama atafaidika na fao hilo mara mara nne.”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Angellah Kairuki (wapili kushoto), akiwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(wakwanza kushoto), wakisikiliza maelezo kuhusu shughuli za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kutoka kwa Afisa Mkuu wa Mafao, PSSSF Bw.Daniel Dugilo (aliyeipa mgongo camera), wakati mawaziri hao walipotembelea banda la PSSSF kwenye viwanja vya Nyakabindi kunakofanyika maonesho ya Nanenane kitaifa Agosti 3, 2020.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Angellah Kairuki (w (kushoto), akiwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(katikati), wakisikiliza maelezo kuhusu shughuli za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kutoka kwa Afisa Mkuu wa Mafao, PSSSF Bw.Daniel Dugilo (aliyeipa mgongo camera), wakati mawaziri hao walipotembelea banda la PSSSF kwenye viwanja vya Nyakabindi kunakofanyika maonesho ya Nanenane kitaifa Agosti 3, 2020.

Aliyekuwa Katibu Tawala mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini (wapili kushoto) akifurahia jambo alipotembelea banda la mfuko huo Agosti 3, 2020.

Kaimu Meneja wa PSSSF mkoa wa Mara, Bi.Nyaswi Elias