*Ampongeza Mhe. Rais kwa kuwezesha hatifungani kutolewa

*Bodi itekeleze majukumu yake vyema, Bodi yaahidi kutekeleza majukuumu kwa uadilifu

*Asisitiza Uwekezaji uwe wenye tija na endelevu,

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kutolewa kwa hatifungani kama malipo ya deni la Serikali kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Profesa Ndalichako alisema hayo Ijumaa, Machi 11, 2022 jijini Arusha alipokuwa akizindua Bodi ya Wadhamini ya PSSSF iliyoteuliwa Disemba mwaka jana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Mha. Mussa Iyombe nyaraka wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSf jijini Arusha, tarehe 11 Machi 2022.

“Tunamshuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya kipindi cha mwaka mmoja amewezesha kutoa trilioni 2.17 kwa ajili ya kulipa deni hilo lililodumu kwa muda mrefu.

Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi aliyoizindua, Mhe. Ndalichako alisema; “Natoa rai kwa Bodi kuhakikisha mnatekeleza majukumu yote. Nawapongeza kwa sababu Mfuko umeendelea kukua, naomba mhakikishe maswala yote ya fedha mnayasimamia vizuri ili tuweze kulipa mafao. Naomba mhakikishe mnawekeza kwenye miradi yenye tija”.

Akizumgumzia uwekezaji, Mheshimiwa Waziri alielekeza uwekezaji uwe kwenye miradi yenye tija na endelevu na Mfuko uendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa kuwekeza kwenye viwanda vyenye uhakika wa kuongeza ajira na vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini.

“Nafahamu mnawekeza katika viwanda, mfano kiwanda cha Karanga (kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro), jana nilivaa viatu vya Karanga, ni vizuri sana, nawapongeza sana. Kiwanda hiki kitasaidia sana wafugaji wetu kuuza ngozi” alifafanua.

Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF, mara baada ya kuzindua Bodi hiyo, jijini Arusha.

Kwa upande wa watumishi wa PSSSF, Mheshimiwa Waziri aliwataka kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano ili kufikia malengo yaliyopangwa.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alimpongeza, Mheshimiwa Prof. Joyce Ndalichako kwa kuteuliwa na Rais, Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu

Akizungumzia utendaji wa Mfuko CPA Kashimba alisema tangu kuanzishwa kwake, Mfuko unatekeleza majukumu yake vyema chini ya usamimazi wa Bodi ya Wadhamini na kuongeza kuwa changamoto zilizokuwa katika mifuko iliyounganishwa zimefanyiwa kazi na sasa wanachama wa PSSSF wanapata huduma bora kwa kiasi kikubwa.

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini iliyozinduliwa inajumuisha; Mhandisi Musa Iyombe ambaye ni Mwenyekiti, pamoja na wajumbe wengine ambao ni; Dkt. Aggrey K. Mlimuka, Bi. Suzan B. Kabogo, CPA Stella E. Katende, Bw. Victor F. Kategere, Bi. Mazoea Mwera, Bw. Thomas C. Manjati, Bw. Said A. Nzori na Bw. Rashid M. Mtima. Bodi ya Wadhamini ya PSSSF imeundwa kwa kuzingatia utatu wa uwakilishi kutoka Serikalini, Wafanyakazi na Waajiri.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako akiongea wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSf jijini Arusha, tarehe 11 Machi 2022

Akizungumza baada ya uzinduzi wa bodi, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Musa Iyombe alisema, “Tunashukuru sana Mhe. Waziri kwa kuja kutufungulia, asante sana. Nakuhakikishia kazi ya Bodi ni kukushauri na maagizo yako yote sisi kama Bodi tutatekeleza pamoja na majukumu yetu kwa uaminifu na uadilifu, tupo makini hatutakuangusha.

Hafla ya uzinduzi wa Bodi ilihudhuriwa na; Profesa Jamal Adam Katundu, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu.

Matukio Katika Picha:

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi CPA. Stella Katende nyaraka wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSf jijini Arusha, tarehe 11 Machi 2022

Wajumbe wa Bodi ya wadhamini wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani).

Menejimenti ya PSSSF, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya PSSSF, baada ya kuzindua Bodi hiyo, jijini Arusha.