WAZIRI  Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amewataka wastaafu na wale wanaotarajia kustaafu kutokubali kushindwa maisha bali wajipe majukumu binafsi yakiwemo ya ufugaji na ukulima.
Pinda ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wadau wa uvuvi jijini Dar es Salaam ambapo alisema wastaafu wengi wanaishi maisha ya tabu baada ya kustaafu kwa sababu ya kukata tamaa kimaisha.
 “Usikubali kukaa tu nyumbani kuangalia TV na kucheza na wajukuu, utaondoka mapema sana, kustaafu sio kuchoka, fanyeni kazi wekezeni kwenye kilimo, wekezeni kwenye mifugo, mimi nafuga nyuki, nalima na pia nina jishugulisha na ufugaji wa samaki wa mabwawa,” alisema Pinda.

Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Pinda