News2019-10-09T05:40:54+00:00
202, 2022

Msemaji Mkuu: PSSSF hongereni kwa kuwafikia Wanachama

February 2nd, 2022|

*Semina itaiongezea uelewa ofisi ya Msemaji *PSSSF kuendelea kukutana na wadau Na Mwandishi Wetu, Morogoro OFISI ya Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali imetoa pongezi kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kusogeza huduma zake karibu na Wanachama wake nchi nzima ikiwemo Pemba, Ifakara, Korogwe na Kahama. Pongezi hizo zimetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Bw. Rodney Thadeus katika semina juu ya huduma, utendaji na mafao yanayotolewa [...]

2401, 2022

PSSSF YAKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI

January 24th, 2022|

PSSSF yakutana na jukwaa la Wahariri Na Mwandishi Wetu. Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, umekutana na wajumbe wa Jukwaa la Wahariri kwa lengo la kuwajengea uwezo wahariri, Januari 22, 2022. Semina hiyo ilikutanisha Watendaji Wakuu wa PSSSF wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Psssf, CPA. Hosea Kashimba na jukwaa la wahariri wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa jukwaa Bw. Salim salim. PSSSF imekuwa na utaratibu wa kukutana na wadau mbalimbali kwa lengo la kuwaelimisha juu ya [...]

1401, 2022

PONGEZI

January 14th, 2022|

Hongera Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb), kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu. Hongera Mhe. Patrobas Katambi (Mb), kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu. Hongera Prof. Jamal A. Kitundu, kwa kuteuliwa [...]

701, 2022

MHAGAMA AFANYA KIKAO NA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU NA TAASISI ZILIZO CHINI YA WAZIRI MKUU

January 7th, 2022|

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini ya Waziri Mkuu zilizopo Dodoma, leo tarehe 05 Januari 2021, katika ukumbi wa jengo la PSSSF lililopo Makole jijini Dodoma. Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Jenisa Mhagama (hayupo pichani). Waziri wa Nchi, [...]

2212, 2021

Serikali, PSSSF wafikia muafaka juu ya deni la trilioni 4.66

December 22nd, 2021|

*Kwa kuanzia wasaini makubaliano ya trilioni 2.17 *Katibu Mkuu: Deni linalipwa kwa utaratibu wa hati fungani maalum *PSSSF: Tutaendelea kutoa huduma bora kwa Wastaafu Na Mwandishi Wetu, Dodoma Wizara ya Fedha na Mipango imetoa pongezi kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo ambayo yamepelekea kuhitimisha suala la muda mrefu kwa deni la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Kauli hiyo ilitolewa na katibu Mkuu wa [...]

512, 2021

PSSSF YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA NBAA ZA UMAHIRI WA UANDAAJI MAHESABU KWA MWAKA 2020

December 5th, 2021|

*Yaongoza upande wa Taasisi za Pensheni na Bima za Afya *Ushindi unaashiria ueledi,nidhamu na umahiri wa Watumishi *Dhamira kuu ni utunzaji makini wa michango ya wanachama na Rasilimali za Mfuko. Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF umetunukiwa tuzo ya umahiri ya uandaaji wa taarifa za fedha kwa mwaka 2020 zilizotolewa jana na NBAA katika hafla maalum iliyofanyika  katika kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo Imekabidhiwa kwa PSSSF na [...]

Go to Top