News

News2019-10-09T05:40:54+00:00
2607, 2021

RC MWANZA: Wekezeni katika miradi rafiki

July 26th, 2021|

*RC: Wekezeni katika miradi rafiki *Msikurupuke kuanzisha miradi, jifunzeni kwanza *Aipongeza PSSSF kwa semina Na Mwandishi Wetu, Mwanza MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amewashauri Wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuwekeza katika miradi waliyoizoea ili waweze kuindesha vyema na kwa faida. Mhandisi Gabriel alisema hayo Jijini Mwanza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wastaafu watarajiwa kwa wanachama wa PSSSF wa mkoa wa Mwanza inayofanyika Julai 26 hadi [...]

2607, 2021

MTAKA: SEMINA ZA WASTAAFU ZIANZE KWA VIJANA

July 26th, 2021|

*Ashauri Watumishi kujipanga vyema kustaafu *Aipongeza PSSSF kwa kuandaa semina *PSSSF: Semina hizi ni endelevu Na Mwandishi Wetu, Dodoma. MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Anthony ameushauri Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuwashirikisha Vijana wanaoanza kazi katika mafunzo ya kujiandaa kustaafu kwani mipango ya kustaafu huanza pale mtu anapoajiriwa. Bw. Mtaka alitoa ushauri huo Jijini Dodoma alipokuwa akifungua semina kwa Wastaafu wataraji wa PSSSF kwa wananchama wa Mfuko huo mkoani Dodoma. Mkuu [...]

2607, 2021

WANACHAMA PSSSF WAASWA KUJUA TAARIFA ZA MICHANGO YAO MARA KWA MARA, WASISUBIRI MUDA WA KUSTAAFU: MAGAWA

July 26th, 2021|

Na Mwandishi wetu Dar es Salaam. WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wameaswa kuwa na utaratibu wa kujua taarifa na mwenendo wa michango yao mara kwa mara tangu siku walipoajiriwa, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Mbaruku Magawa amesema. Bw. Magawa ameyasema hayo  leo Julai 7, 2021 alipokuwa akitoa tathmini yake ya huduma zinazoendelea kutolewa na Mfuko kwa wanachama, wastaafu na wanaanchi kwa ujumla kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya [...]

2607, 2021

PSSSF YAWASHUKURU WANACHAMA, WASTAAFU NA WANANCHI KWA KUJITOKEZA KWA WINGI KWENYE BANDA LAO WAKATI WA MAONESHO YA SABASABA 2021

July 26th, 2021|

NA MWANDISHI WETU DAR ES SALAAM MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umewashukuru wanachama, wastaafu na wananchi kwa ujumla kwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma wakati wa Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyofikia kilele Julai 13, 2021. Akitoa tathmini ya huduma ambazo zilitolewa na wafanyakazi wa Mfuko wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa [...]

507, 2021

WAZIRI MHAGAMA ARIDHISHWA UTENDAJI WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YA PSSSF NA NSSF

July 5th, 2021|

Na mwandishi wetu Dar es Salaam WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana  na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema katika siku 100 za utawala wa Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan kumekuwepo na mafanikio makubwa ya kiutendaji ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Waziri Mhagama aliyasema hayo leo Julai 5, 2021 alipotembelea banda la [...]

3006, 2021

MAONESHO YA 45 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM: PSSSF YAJA KIVINGINE, WANACHAMA NA WANANCHI WAKARIBISHWA KUPATA TAARIFA ZA KUMILIKI NYUMBA

June 30th, 2021|

Na mwandishi wetu Dar es Salaam MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umewaalika wanachama wake na wananchi kwa ujumla kutembeela banda la Mfuko huo ili kupata taarifa za huduma mbalimbali zikiwemo zile la kumiliki nyumba kwa gharama nafuu. Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw.James Mlowe (kulia), akimpatia Mfuko wenye taarifa mbalimbali za Mfuko Bw. Philipo John aliyefika kwenye Banda la PSSSF kwenye [...]

Load More Posts