*Aitaka Mifuko kuendelea kutoa huduma bora

*Azitaka Bodi zisimamie uwekezaji wenye tija

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kuhakikisha waajiri wote wanawasilisha makato ya watumishi kwa ajili ya pensheni zao.

Mhe. Mhagama alisema hayo mwishoni mwa wiki jijini Mwanza wakati akifunga mkutano wa shirikisho la mashirika ya Hifadhi ya jamii nchini.

“Mifuko inawajibu mkubwa wa kuhakikisha Waajiri wanaandikishwa na wanalipa michango kwa wakati. Idadi ya Waajiri ambao hawalipi michango imeongezeka hususani makampuni ya Ulinzi” alisisitiza Mhe. Mhagama.

Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa kufunga semina ya wajumbe wa Shirikisho la Mashirika ya Hifadhi ya Jamii (TSSA) walipokutana tarehe 19 Desemba, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Gold Crest Jijini Mwanza.Mkutano ulihudhuriwa na Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi mbalimbali wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko hiyo.

Mhe.Waziri ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuhakikisha kabla ya mwanachama hajastaafu nyaraka zake zinakuwa sawasawa ili kumwondolea usumbufu mwanachama ambaye amelitumikia taifa kwa muda mrefu.

Pia Mhe Waziri ameitaka Mifuko kuendelea kufanyakazi vizuri, kwa lengo la kuwahakikisha wanachama maisha bora baada ya kustaafu, na kuongeza “Niwapongeze sana kwa hilo, kwani sisi kama Wizara tunaamini kuwa unapomwezesha mwanachama kuwa na uhakika wa kesho atafanya kazi kwa utulivu hivyo kuweza kuzalisha kwa tija na ufanisi”.

Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa kufunga semina ya wajumbe wa Shirikisho la Mashirika ya Hifadhi ya Jamii (TSSA) walipokutana tarehe 19 Desemba, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Gold Crest Jijini Mwanza.Mkutano ulihudhuriwa na Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi mbalimbali wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko hiyo.

Mhe. Waziri ameitaka Mifuko kuendelea kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wanachama wake kwa lengo la kuondoa dosari ambazo zipo.

Katika hatua nyingine Mhe. Wazri amezitaka bodi za wadhamini ziendelee kusimamia vyema na kwa uadilifu Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika maeneo wanayowekeza ili uwekezaji huo uwe na tija kwa wanachama wake.

“Jukumu lingine zito linalofanywa na bodi zetu ni kushauri na kusimamia uwekezaji unaofanywa na mifuko ya hifadhi ya Jamii kwa lengo la kulinda pesa za wanachama. Sote tunatambua kuwa sera ya Serikali ya awamu ya tano ni uchumi wa Viwanda kama dira ya miaka mitano iliyopita na miaka mitano tuliyoianza sasa, ilani ya Chama cha Mapinduzi kuanzia 2020 hadi 2025. Inatuelekeza kufanya uwekezaji makini katika viwanda” alifafanua Mhe. Mhagama.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini (TSSA) Bw. Meshack Bandawe,akizungumza kuhusu shirikisho la Mifuko hiyo wakati wa mkutano wao mara baada ya kuhitimisha mafunzo ya siku Tatu mkoani Mwanza.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatulia hotuba ya Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatulia hotuba ya Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.

Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Hosea Kashimba.

Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha ushiriki Mwenyekiti wa Shirikisho la Mashirika ya Hifadhi ya Jamii (TSSA) Bw.William Erio mara baada ya kuhitimisha wa mafunzo kwa wajumbe wa Shirikisho hilo.

Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Sekretarieti walioandaa semina hiyo iliyowakutanisha Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi mbalimbali wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko hiyo.

Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya PSSSF.

Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Mfuko wa PSSSF.