Na Mwandishi wetu, Morogoro

Maafisa wa wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi sasa watapatiwa elimu ya maandalizi kustaafu katika maeneo wanayofanyia kazi katika ngazi ya wilaya na mkoa.

Hilo lilikuwa ni moja maazimio ya semina ya mafunzo maalum kwa watumishi wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi, iliyoratibiwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kushirikiana na wizara ya mambo ya ndani na idara zake zote iliyofanyika mwishoni mwa Agosti 2019 mjini Morogoro.

Elimu hiyo ya maandalizi ya kustaafu itatolewa na maafisa wa wizara ya mambo ya waliopatiwa mafunzo maalum na PSSSF, lengo ni kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa kabla ya watumishi wa wizara hiyo kustaafu.

Maazimio mengine ya kikao hicho ni; mwajiri kuhakikisha anawasilisha nyaraka za watumishi wanaotarajia kustaafu miezi sita kabla ya kustaafu, Mfuko kufanyia marekebisho ya fomu mbalimbali ikiwemo kutafsiri fomu za mafao mbalimbali kutoka lugha ya Kiswahili kwenda kiingereza, Mfuko kusafisha taarifa za wanachama na maafisa watakao kuwa wanashughulikia mafao ya watumishi wapatiwe vitambulisho ili wajulikane.

Lengo la semina hiyo lilikuwa kutengeneza uelewa juu ya sheria na kanuni zinazoongoza Mfuko kwa lengo kupunguza ucheleweshwaji wa malipo ya mafao ya wanachama ambao ni watumishi wa wizara ya mambo ya ndani.

Katika semina hiyo mada zilizowasilishwa ni pamoja na; Historia ya Hifadhi ya Jamii, Sera,Sheria na kanuni za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Wajibu wa Serikali, Mwajiri, Mfuko na Mwanachama, Michango ya mwanachama, Uwasilishaji wa michango kupitia GePG, Elimu na umuhimu wa maandalizi ya kustaafu, Mafao yanayotolewa na Mfuko na Ukokotoaji wa mafao.

Semina hiyo iliyofungwa Agosti 30, 2019 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani Bw. Rajabu kailima ni matokeo ya kikao kati ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Kashimba Hosema na Bw. Kailima ambacho kilijadili juu ya changamoto mbalimbali. Katika semina hiyo ya Morogoro, Mfuko uliwakilishwa na Bw. Ansigar Mushi, Mkurugenzi na Tathimini na hadhari.

Wakati huohuo Mwandishi Wetu kutoka Dodoma anaripoti kuwa, Mfuko uliendesha semina kwa Mameneja wa Mfuko kutoka ofisi mbalimbali za Mfuko nchini kwa lengo la kuwapatia ulewa wa  Mfumo wa Malipo wa Kieroktroniki wa malipo ya Serikali (GePG).

 

Mkurugezi Mkuwa PSSSF, Bw. Hosea Kashimba alimsikiliza kaimu Meneja wa Mfuko mkoa wa Singida Bi. Beatrice James.

Akizunguzia mfumo huo, Kaimu Mkrugenzi wa Fedha Bibi. Beatrice Lupi, alisema kwa upande wa PSSSF, mfumo huu hutumika katika ukusanyaji wa michango ya wanachama, mapato ya uwekezaji na mapato mengine. PSSSF kama moja ya taasisi ilijiunga na mfumo huo tangu Februari 2019.

Mkurugenzi huyo alisema GePG ina faida zilizogawanyika katika makundi mawili, kwa upande wa waajiri faida ni: kujifanyia tathimini ya michango inayoletwa PSSSF, kujitengenezea ankara za malipo, kuweza kupata risiti kwa wakati,kulipa michango wakati wowote, kupunguza safari za kwenda kwenye ofisi za Mfuko kwa huduma mbalimbali na Kutunza kumbukumbu ya ankra na risiti zote za michango katika mfuko.

Bibi. Lupi alizitaja faida kwa upande PSSSF kuwa ni pamoja na: kuongeza uwazi, kuongeza ufanisi wa ufuatiliaji wa michango kwa waajiri, kukusanya michango kwa wakati na Kuwezesha Mfuko kufanya ulinganifu wa michango. Semina hiyo ilifanyika Septemba 2-5, 2019 jijini Dodoma.

 

Kaimu Mkrugenzi wa Fedha Bibi. Beatrice Lupi, akitoa ufafanunuzi katika kikao hicho.