Kashimba: Tuendelee kutoa elimu ya Mafao na Huduma

Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Kikao cha nane cha Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kilihitimishwa Februari 5, 2021 mjini Morogoro kwa Mwenyekiti wake CPA. Hosea Kashimba amewataka watumishi kuendelea kutoa elimu ya Mafao na huduma zinatolewa na Mfuko.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja pembeni mwa kikao hicho katika ukumbi wa Magadu, Mjini Morogoro.

“Tuendelee kutoa huduma bora kwa wanachama wetu wote, pia tusisahau kuwaelimisha juu ya Mafao na huduma tunazotoa hususani kwa wanachama wanaokaribia kustaafu ili waweze kujipanga vyema” alisisitiza Bw. Hosea ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF.

Katika kikao hicho cha nane cha baraza, wajumbe walijadili hoja kutoka Kurugenzi, Kanda na vyama vyama vya wafanyakazi vya TUICO na TALGWU. Pia wajumbe walipitia taarifa ya utendaji wa Mfuko ya nusu mwaka kutoka Julai hadi Desemba, 2020.

Wataalam kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Bi. Sarah Martine (kulia) na Bw. Bigambo James wakitoa mada ya Mapambano dhidi ya Rushwa katika baraza wafanyakazi wa PSSSF linaloendelea mjini Morogoro.

Baraza lilhudhuriwa na Bw. Willy Kibona kutoka TUICO makao makuu, Bw. Rajabu Jana kutoka TUICO Dodoma na Bi. Happynes Makombe kutoka TALGWU, Dodoma.

Wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa PSSSF wakifuatilia kikao cha Baraza.

Kikao cha baraza la wafanyakazi ni kikao cha kikanuni ambacho kila taasisi inapaswa kukiitisha kwa lengo la kuwashirikisha watumishi katika maamuzi na kusikiliza hoja kutoka kwa watumishi.