Dkt. Malaba: Tuwe makini na afya zetu

*Tubaini magonjwa mapema, tufanye mazoezi, tule vyakula bora

*Bajeti ya Mfuko ya 2021/22 yawasilishwa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kikao maalum cha tisa na kumi cha baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam ambapo watumishi wa Mfuko wameshauri kuwa makini na afya zao ili waweze kuwa na afya njema kwa maslahi ya Mfuko, familia zao na taifa kwa jumla.

Hayo yalisemwa na Dkt. Raphael Malaba kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) alipokuwa akitoa elimu juu ya magonjwa yasiambukizwa kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko.


Dkt. Raphael Mabala kutoka NHIF, akitoa mada ya Bima ya Afya na magonjwa yasiyoambukizwa.

“Ni vyema kubadili mfumo wa maisha kwa kula vyakula bora, kupuguza unene, kufanya mazoezi, kuacha au kupunguza unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara na kubaini magonjwa mapema”.

Dkt. Malaba alisema ni vyema kuwa makini na afya zetu kwani matibabu ya magonywa yasiyoambukizwa yanatibika kwa gharama kubwa. Hivyo tukiwa makini tutajipunguzia gharama wenyewe na taifa kwa jumla.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba akiongoza kikao cha Baraza. Kushoto ni Katibu wa kikao hicho Bw. Steven Biko na kulia ni katibu Msaidizi Bi. Linda Njoolay.

Katika hatua nyingine; Mkurugenzi wa fedha wa Mfuko Bibi. Bearece Musa-Lupi aliwasilisha bajeti ya Mfuko ya mwaka 2021/22 ili ijadiliwe na Wajumbe wa Baraza kabla ya kuwasilishwa kwa mamlaka nyingine ikiwemo Bodi ya Wadhamini wa Mfuko.

Katika kikao cha kumi wajumbe walifanyia kazi agenda zifuatazo; kuthibitisha mihutasari ya vikao vya kawaida vya saba na nane na taarifa ya mpango na bajeti kwa mwaka 2021/2022.

Mkurugenzi wa Fedha, Bibi. Beatrice Musa-Lupi akiwasilisha bajeti ya Mfuko kwa 2021/2022.

Bw. Juma Milinga, Mwenyekiti wa TALGWU tawi la PSSSF, akichangia hoja katika Baraza.

Wajumbe wa Baraza Bw. Godfrey Mvena na Bw. Salvatory Rugumisa wakifatilia kikao cha Baraza.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza wakifuatilia kikao.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza wakifuatilia kikao.

Mjumbe wa Baraza Bw. Mohamed Madenge akifungua kwa sala.

Mjumbe wa Baraza Bi. Grace Fihavango akifungua kwa sala.

Wajumbe wa Baraza wakiwa katika picha ya pamoja.

Wajumbe wa Baraza wakiwa katika picha ya pamoja.